Home Mchanganyiko Vijana wa Dar Changamkieni Fursa

Vijana wa Dar Changamkieni Fursa

0

************************

Nteghenjwa Hosseah, Dar es salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(Mb) amewataka vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam kuchangamkia fursa za mikopo ya vijana inayotolewa katika kila Halmashauri Nchini.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati alipokua akifungua Kampeni ya Vijana Twende inayolenga Vijana wa Dar es salaam kuchangamkia fursa za kujukwamua kiuchumi iliyofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika ufunguzi huo Waziri Jafo amesema Kampeni ya Vijana Twende itasaidia kuhamasisha vijana wa Mkoa wa Dar es alaam kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazotolewa na Serikali, ikiwemo mikopo ya vijana (4%) kutoka halmashauri za jiji la Dar es salaam pamoja na zile zinazotolewa na wadau wangine wa maendeleo.

« Msingi mkuu wa kampeni hii ni kubadili fikra na tabia za vijana na kuwafanya vijana Kuwa na uwezo wa kutengeneza makundi ya kuwazalishia kipato na Kuwa na vijana wenye maadili ya kuchapa kazi,kutokutukutumia madawa ya kulevya, wasiowazembe, wanaojali muda na wenye matumizi ya fedha yenye tija.

Aliongeza kuwa tunataka tupate vijana walioungwa katika duru za maamuzi katika ngazi mbalimbali kuanzia mtaa,kata,wilaya,mkoa na Vijana wanaoshiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii » alisema Jafo

Kwa Kampeni hii napenda kutambua mchango wa Shirika la Baba Watoto Organisation kupitia Ufadhili wa shirika la Foundation for Civil Society (FCS) ambao umewezesha kufanyika kwa shughuli mbali mbali za mradi na vijana wengi kuhamasishwa na kujengewa uwezo katika kuchangamkia fursa za kiuchumi ili kupunguza tatizo la ajira na kiwango cha umaskini katika nchi yetu.

Alimalizia kwa kusema kuanzia sasa sina mashaka na vijana wa Dar es salaam naamini kupitia Kampeni hii watakua wamepata uelewa wa kutosha wa namna ya kupata mikopo inayotolewa na Serikali na ile ya wadau.

Akizungumza katika Kampeni hiyo Meneja Programu toka Foundation for Civil Society Francis Uhadi amemuomba Waziri Jafo kuwa ikiwezekana idadi ya vijana wanaotakiwa kujiunga katika makundi ili kuomba mikopo kwenye Halmashauri ipungue kutoa vijana kumi hadi kufikia watano ili kurahisisha upatikanaji wa vijana hao.

Aliongeza kuwa muda wa kuomba hadi kupatiwa mikopo hiyo uwe mfupi kidogo kwani kwa sasa huwa inachukua miezi sita hadi mwaka hivyo kuwakatisha tamaa waombaji.

Naye Mkurugenzi wa Baba Watoto Organisation Oscar Kapande amesema shughuli za mradi wa Vijana Twende zimetekelezwa katika Miji nane(8)ya Tanzania Bara na Zanzibar ikiwemo Mbeya, Dodoma, Mwanza, Arusha, Longido ,Unguja,Pemba na Dar es salaam.

Ameongeza kuwa haya ni maono muda mrefu ya Shirika hilo ya kuhudumia vijana katika nyanja mbali mbali za Maisha, pamoja na kuchukua hatua hii ya kuhamasisha na kujengea uwezo vijana kuchangamkia fursa za kiuchumi.