**************************
Na Ahmed Mahmoud Arusha
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju juzi (jana) amezindua Jukwaa la Haki Jinai la Mkoa wa Arusha ili kuharakisha utoaji wa haki kwa watu mahakamani na mahabusu.
Akizungumza jana katika hafla fupi ya uzinduzi wa jukwaa hilo, Mpanju alisema kufungulia kwa jukwaa hilo kutasaidia kupunguza hata mlundikano wa mahabusu gerezani, ambako rais John Magufuli aliagiza walishulikie.
”Mi nawapongeza sababu hii ni moja ya hatua ya kushughulikia changamoto hii na zingine na atu atapata haki kwa wakati,”alisema.
Aidha aliagiza wajumbe wa Jukaa hilo ambao ni viongozi wa vyombo vya Ulinzi na usalama, kuongea kasi ya kushughulikia wale wote anaohujumu serikali kwa ajili ya maslahi yao binafasi.
“Msiogope mtu yoyote menye cheo chochote ili mradi hamumwonei mtu, tekelezeni majukumu yenu ka kuisaidia serikali na kama hapa Arusha nawapongeza maana mlishakamata watoroshaji a madini ya Tanzanite waliokuwa akipeleke nchini Kenya na kuchangia pato la taifa kwa kupata madini hayo,”alisema
Alisema Arusha ni kitovu cha utalii,madini mengi na mikutano ya kimataifa mingi, hivyo kuna kila haja ya kuimarisha ulinzi ili kuwe na amani na usalama,”alisema
Kuhusu uchaguzi aliagiza kila mwananchi kufuata sheri na taratibu za nchi, ili wawe salama katika kuedesha shughuli zao za kiuchumi na kua makini katika kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka huu, kwa kukwepa kufanya makosa ya jinai.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka nchini (DPP), Biswalo Mganga alisema anaamini Jukwaa hilo litasaidia kupambana na uhalifu mkoani hapo.
“Naamini huwezi kua na maendeleo bila kua na haki au kutenda haki kwa watu, hivyo kupitia jukwaa hili watu watapata haki zao kwa haraka na kupunguza malalamiko ya kuchukua muda mrefu mashauri,”alisema.
Aliagiza viongozi a Jukwaa hilo kuhakikiha wanahudhuria vikao viwili vya lazima kila mwaka bila kutuma wawakilishi ili kupanga mikakati ya kushughulikia uhalifu katika eneo lao.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Longido Franck Maisumbe aliyehudhuria hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, alishukuru jukwa hilo kuzindulia mkoani hapo na kuahidi kutoa ushirikiano ili kazi zilizokusudiwa zifanikiwe.
Pia alipongeza ofisi ya DPP kuondoa urasimu na kuharakisha mashauri kwa ajili ya kutoa haki ka wakati ka ananchi.
“Natarajia jukwaa hili litakua msaada kwa Wilaya, Mkoa na Taifa katika kupunguza kero za wananchi katika mashauri yao, sababu wananchi wanapochelewa kupata haki wanaanza kuichukia serikali na kuilaumu,”alisema