Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dk John Pima (kulia) wakielekea kwenye kikao cha Baraza la Madiwani jana.
Vijana wa Skauti wakimisha skafu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu kabla hajaelekea kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua jana.
Baadhi ya Madiwani, Walimu na wananchi wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua jana ambacho pamoja na ajenda nyingine Baraza lilitoa fedha taslimu kwa Shule za Msingi na Sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa ya 2029.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kaliua Haruna Kasele( wa tatu kutoka kulia) akisoma dua kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Madiwani jana.
.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dkt. John Pima akijibu maswali ya papo kwa papo ya Madiwani wakati wa kikao cha Baraza Madiwani kilichafanyika jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dkt. John Pima (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Kaliua Magdalena Sakaya (kulia) wakijadiliana jambo wakati wa kikao cha Baraza Madiwani kilichafanyika jana.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kaliua Haruna Kasele akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika jana.
NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua imetoa shilingi milioni 10 za motisha na vyeti kwa shule za msingi na sekondari zilizofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dkt. John Pima wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo.
Alisema kuwa lengo la kutoa fedha hizo ni kutoa motisha kwa ajili ya kuwahamisha walimu waongeze juhudi ili kuondoa daraja sifuri na daraja la nne.
Dkt. Pima alisema motisha hiyo imezingatia shule zenye ufaulu kwa alama A, ufaulu wa somo kwa A na B pekee, shule zenye ufaulu wa wastani wa B na shule zenye ufaulu bila Daraja sifuri.
Alisema kuwa walipoanzisha mpango huo walianza na kutoa motisha jumla ya shilingi milioni 1 na sasa hivi wameamua kutoa milioni 10 na wanatarajia kuongeza hadi kufikia milioni 30.
Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu aliwataka walimu kuhakikisha wanaondoa Daraja sifuri na la nne mkoani humo.
Alisema sio jambo la kupendeza kuona kuwa mwalimu amekaa na mwanafunzi kwa kipindi cha miaka minne mwisho wake anapata daraja sifuri.
“Hata shule za Sekondari ambazo wanafunzi wanafanya vizuri walimu ni sawa na wao na wamesoma katika vyuo ambao nao wamesoma, hivyo hakuna sababu ya wanafunzi kufanya vibaya”alisema.