Home Siasa CCM KIBAHA MJINI YAWAWEKA KITIMOTO WAPIGA DEBE WA WAGOMBEA- LUAMBANO

CCM KIBAHA MJINI YAWAWEKA KITIMOTO WAPIGA DEBE WA WAGOMBEA- LUAMBANO

0

**************************

28,feb

NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
KATIKA kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao ,Chama Cha Mapinduzi (CCM),mjini Kibaha kimeanza kuwachukulia hatua baadhi ya wapambe wa wagombea ,wanaojipitisha kuwapigia debe wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi .
Aidha chama hicho kimepiga marufuku wagombea wanaojipitisha na wapambe wao ,kuacha mara moja kufanya hivyo kwani wanakiuka taratibu na maadili ya chama.
Akitoa taarifa kuhusiana na mkutano mkuu wa jimbo ,unaotarajia kufanyika march 2 mwaka huu,mjini Kibaha ,kwa lengo la mbunge wa jimbo hilo Silvestry Koka kueleza utekelezaji wa ilani, katibu wa CCM Kibaha Mjini ,Afidh Luambano alisema ,hadi sasa wamekaa vikao na kuwaonya wale waliosikika kujipitisha kuwanadi wagombea wao.
“Hizo ni vurugu ,waache madiwani na mbunge aliyepo madarakani wafanye kazi na kumaliza muda wake ,waache kujipenyeza penyeza kwasasa sio muda wao”alifafanua Luambano.
Luambano alieleza ,chama hicho kitaendelea kusimamia msingi na haki na wamejipanga kushinda kata zote na jimbo na Rais katika uchaguzi huo.
Pamoja na hayo ,alielezea katika mkutano mkuu wa jimbo ,mgeni rasmi anatarajiwa kuwa katibu mkuu Taifa ,Bashiru Ally ,na wamealikwa mabalozi wote mjini hapo 599, wenyeviti 73 na viongozi maarufu.
Akizungumzia mtaji wa chama kuongeza wanachama wapya alisema ,mwaka 2018 kulikuwa na 39,000 na hadi kufikia 2019 waliongezeka na kufikia 53,230.
“Katika uchaguzi wa serikali za mtaa,vijiji na vitongoji waliongezeka na kufikia 53,230 na hadi sasa waliongizwa katika mfumo wa kielektronik ni wanachama wapya 10,824 ambao wamelipia ada sh.milioni 8.927.168.”alibainisha Luambano.