Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu akisalimiana na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Kiromba,kata ya Kiromba,Wilaya ya vijijini,Mkoa wa Mtwara wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme kijiji humo.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu(aliyeshika mkasi) akikata utepe kuashiria kuwashwa kwa umeme katika kijiji cha Kiromba,kata ya Kiromba,Wilaya ya Mtwara vijijini Mkoa wa Pwani.
Bi Zahara Juma(aliyeshika kipaza sauti)wa kijiji cha Mwenge kilichopo kata ya Kiyanga, Wilaya ya Mtwara vijijini, Mkoa wa Mtwara, akitoa neno la kushurani mara baada ya kuwashiwa umeme kwenye kijiji chao.
Wananchi wa kijiji cha Ushirika, kata ya Mangochapanne wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu(hayupo pichani) kwenye mkutuno wa hadhara uliofanyika kijijini humo.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akiongea na wananchi wa kijiji cha Mwenge,kata Kiyanga,Wilaya ya Mtwara vijijini,Mkoa wa Pwani (hawapo pichani) wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme kijiji humo.
***************************
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema Serikali kupitia Wizara ya Nishati na taasisi zake zinazohusiana umeme zimejipanga kikamilifu kuhakikisha inaziondoa kasoro ambazo zilijitokeza kwenye miradi ya REA iliyopita.
Ayasema hayo,Februari 26,2020, wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kiromba,Kata ya Kiromba,Wilaya ya Mtwara vijiji,Mkoani Mtwara,kabla ya kuwasha umeme kwenye kijiji hicho.
Amezitaja baadhi kasoro hizo nia pamoja na baadhi ya wakandarasi kupewa maeneo makubwa ya mikoa miwili hadi mitatu tofauti yenye ukubwa tofauti, ambapo ilipelekea baadhi ya wakandarasi wengine kutokufanya kazi kwa ufanisi na kasoro nyengine iliyojitokeza kwenye miradi hiyo ni kurukwa kwa baadhi ya vijiji.
Aidha, alisema Serikali inataka mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili uondoe kasoro zilizokuwepo kwenye REA zilizopita na mradi wa REA unaoendelea,Serikali imeamua kwamba, vijiji vyote lazima vipangwe kimajimbo na kusisitiza kuwa hawatakubali kuona baadhi ya vijiji vya nyuma vikiachwa na kupelekewa umeme na kupelekewa umeme vijiji ambavyo vipo mbele.
Ameongeza kuwa, Serikali itakerebisha mapungufu mbalimbali yaliyojitokeza kwenye miradi ya REA iliyopita ili mradi wa REA III mzunguko wa pili ufanyike kama ufanisi na tayari hatua za kutatua kasoro hizo zimeanza kuchukuliwa
“kwenye mradi wa Peri-Urban tulifanya kila wilaya na mkandarasi wake,kila mkandarasi amejielekeza kwenye wilaya yake hii imesaidia sana, na katika mchakato wa REA III awamu ya pili Serikali inadhamiria kupitia sheria za manunuzi kwamba walau kila mkandarasi apewe kiasi anachokimudu kwa wakati ule kwasababa hatuna muda mwingi na tunatakiwa 2021 tukamilishe kazi”
Pia,amewatoa hofu wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa kuwaeleza kuwa maeneo yote ambayo bado umeme haujafika yataingizwa kwenye orodha ya kazi zinazoendelea na kuwahakikishia kuwa fedha zipo kupitia mfuko wa Nishati vijijini na kupitia wadau mbalimbali wa maendeleo ambao wameridhishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ili kuwaletea maendeleo Watanzania.
Vilevile, amesema Serikali haitakubali kuona tena maeneo ambayo yapo barabarani lakini hayana umeme, amesema kuwa maeneo yote kama hayo yanatakiwa kupelekewa umeme kwa haraka zaidi.
Aidha, alisema mwakani mara tu baada ya kumalizika kwa mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili, Serikali itaanza kazi ya kupeleka umeme kwenye vitongoji na kazi hiyo itakuwa ni rahisi kwasababu umeme mkubwa utakuwa umefika kwenye kila kata.
Nae Bi Zahara Juma ambae ni mwanakijiji cha kijiji hicho ambae amejiajiri kwenye duka la madawa amesema Serikali iendelee kusambaza umeme vijiji,bila ya umeme huduma za kijamii huwa zinatolewa na tabu, pia ameishukuru Serikali kwa kupeleka umeme kwenye kijiji chao ambapo amesema saivi ataweza kuwauzia dawa wanakijiji wenzake hata mda wa usiku.
Katika ziara yake hiyo, ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme vijijini ,Naibu Waziri wa Nishati, pia aliwasha umeme katika vijiji vya Mwenge, kata ya Kiyanga,kijiji cha Ushirika kata ya Mangopachanne na kijiji Kitere kata ya Kitere, wilaya ya Mtwara vijijini,Mkoa wa Mtwara.