Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Bw. Biswalo Mganga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Mahakama na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto kwake) baada ya kuzindua Jukwaa la Haki Jinai hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Bw. Biswalo Mganga (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, baada ya kuzindua Jukwaa la Haki Jinai hivi karibuni.
Na Ismail Luhamba, Singida
AKIWA kwenye ziara ya kikazi mkoani Singida Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Bw. Biswalo Mganga amewataka wakuu wa mikoa nchini kote kufanya uzinduzi rasimi wa majukwa ya haki jinai katika mikoa yao ilikuyapa nguvu majukwa hayo ya kufanya kzi kwa ufanisi.
Ameyasema hayo mkoani singida wakati wa hafla ya uzinduz wa Jukwaa la Haki Jinai katika mkoa wa Singida hafla iliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa mkoa mkoani hapa jana.
Akifafanua kuhusu majukwaa ya haki jinai Mganga amesema lengo ni kuhakikisha shughuli za kijinai ndani ya mkoa zinakwenda vizuri
Amesema azma yake hasa ni kuweka stratejia, kuratibu, kubuni na kuhakikisha mwenendo mzima wa makosa ya kijinai yanaratibiwa kwa ufanisi mkubwa
“Mathalani changamoto kama mlundikano wa mahabusu kwenye vizuizi vya polisi au magerezani ni mojawapo ya jukumu la jukwaa hili katika ufuatiliaji wa karibu zaidi,”
Aidha, Mganga ameongeza kuwa majukwaa haya kwa mujibu wa sheria yana haki ya kuleta mapendekezo katika ofisi ya taifa ya mashtaka yanapoona inafaa hususan kwenye eneo la mabadiliko yoyote yanayoweza kuleta tija kulingana na jiografia ya sehemu husika
Sambamba na hilo, akiwa ziarani mkoani hapa amefuta kesi 85 zinazohusiana na rushwa na udanganyifu ndani ya gereza la Manyoni, ikiwa ni mwendelezo wa juhudi za serikali katika kupunguza mlundikano wa mahabusu magerezani
“Kuanzia majira saa 5 asubuhi jana mpaka saa 12 jioni nilipata nafasi ya kusikiliza baadhi ya mahabusu wa gereza la manyoni na mwisho kwa wale waliokiri kuwa wamefanya makosa hayo na hawatarudia tena nikaamua kufuta kesi hizo zipatazo themanini na tano,” amesema Mganga
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amesema uwepo wa Jukwaa la haki jinai ngazi ya mkoa ni kuongeza usalama na amani ndani ya mkoa husika
Amewataka wajumbe wa jukwaa hilo kufanya kazi kwa umoja na uzalendo wa hali ya juu ili kuhakikisha uhalifu na viashiria vyake ndani ya mkoa vinapungua na kufutika kabisa
“Tafsiri ya Jukwaa hili ni ile ile azma ya Mheshimiwa Rais ya kuendelea kuwajali, kuwathamini na kuwapenda wananchi wake, kwa maana ya chachu na njia ya kutuepusha na uhalifu,” amesema Nchimbi
Akitoa neno la shukrani, Mwenyekiti Mteule wa Jukwaa la Haki Jinai mkoani hapa, Rose Chilongozi alisema chombo hicho kitaangalia namna ya kujikita katika kutoa elimu kwenye Nyanja mbalimbali
“Ni ushirikiano pekee kwa kila mtu kwa nafasi yake ndio utakaotuwezesha kukabiliana kikamilifu na uhalifu…ni fursa ya wateuliwa kukaa pamoja kwa umoja na kutafakari na kuweka mikakati,” amesema Chilongozi
Mmoja wa wajumbe wa Jukwaa hilo, ambaye ni Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Singida, Safina Muhindi amesema chombo hicho kinakwenda kurahisisha na kuwezesha ushahidi kupatikana kwa urahisi na uendeshaji wa mashauri ya kijinai kuwa wa haraka zaidi,” amesema Muhindi