Klabu ya Mbao FC kutoka jijini Mwanza imemrejesha aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Kikosi hicho Abdulmutik Haji katika Kikosi hicho kuwa Kocha Mkuu
Abdulmutik na Kocha Mkuu Hemed Morocco waliachana na Klabu hiyo hivi karibuni kwa makubaliano ya pande zote mbili kutokana na matokeo mabaya.
Katibu Mkuu Wa Klabu Hiyo Daniel Naila amesema kuwa wameamua kumrejesha Haji ili kuinusuru Mbao FC kwani tayari Mbinu na Falsafa zake Ziliaanza kupokelewa na Wachezaji hivyo anaamini Itakuwa rahisi kuliko Kumuajiri Mwalimu Ambaye ataanza Upya kabisa .
Haji ataendelea na mkataba wake wa awali mkataba ambao unaisha mwisho wa msimu huu huu.
Timu ya Mbao ipo katika hali mbaya ya kushuka daraja kutokana na kuwa na matokeo mabovu na kuendelea kujiweka katika hali tete zaidi hivyo wanatakiwa kupambana kweli kweli ili wabaki Ligi Kuu msimu ujao.