Home Biashara KANZIDATA YA KUDUMU YA WATOA HUDUMA ZA FEDHA ITASAIDIA KUKUSANYA TAARIFA ZA...

KANZIDATA YA KUDUMU YA WATOA HUDUMA ZA FEDHA ITASAIDIA KUKUSANYA TAARIFA ZA KIFEDHA

0

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,Profesa Florence Luoga, (kushoto),akibofya kitufe maalum wakati wa uzinduzi wa Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma za Fedha katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar Es Salaam leo,Katikati ni mwakilishi wa chama cha wamiliki wa makampuni ya simu nchini  Epimack Mbeteni, ambaye ni mkurugenzi wa  Vodacom M-pesa   na Naibu Mrajisi wa tume ya maendeleo ya ushirika,Collins Benedict.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,Profesa Florence Luoga, (kulia),akiongea na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo,  wakati wa  hafla ya uzinduzi wa Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma za Fedha.  Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, Bw.Benard Dadi ,Benard Dadi,Mkurugenzi Mkuu wa FSDT ,Sosthenes Kewe  watatu (kushoto) na mwakilishi wa chama cha wamiliki wa makampuni ya simu nchini  Epimack Mbeteni

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,Profesa Florence Luoga, (kulia),akiongea na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo,  wakati wa  hafla ya uzinduzi wa Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma za Fedha.Katikati ni  Naibu Gavana wa Benki Kuu,Dk.Benard Kibesse na  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB Community bank, Godfrey Ndalahwa.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,Profesa Florence Luoga, (wa tatu kushoto),akibofya kitufe maalum wakati wa uzinduzi wa Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma za Fedha katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar Es Salaam leo,(wa pili kushoto) ni Naibu Gavana wa Benki Kuu,Dk.Benard Kibesse,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB Community bank, Godfrey Ndalahwa,wengine kutoka kulia ni Meneja Usimamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa  Huduma za Bima (TIRA),Paul Abdiel , Naibu Mrajisi wa Tume ya maendeleo ya ushirika,Collins Benedict na ni mwakilishi wa chama cha wamiliki wa makampuni ya simu nchini  Epimack Mbeteni, ambaye ni mkurugenzi wa  Vodacom M-pesa

…………………………………………

Gavana wa BoT, Profesa Florence Luoga, amesema  kanzidata ya watoa huduma za kifedha nchini (FSR), ambayo imetayarishwa na BoT kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) itasaidia kukusanya taarifa mbalimbali za kifedha mara baada ya watoa huduma za kifedha nchini kusajiliwa katika Kanzidata hiyo.

Gavana Profesa Luoga amesema usajili wa watoa huduma za fedha nchini, utaanza mwezi Machi hadi Juni mwaka huu na utahusisha makundi mbalimbali ya watu hao.

 Gavana Profesa Luoga amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kanzidata hiyo itakayosajili watoa huduma za kifedha  ulifanyika ukumbi kwenye wa BoT.

Amesema FSR ni daftari la kwanza la aina yake barani Afrika chini ya Jangwa la Sahara, ambalo litakuwa na takwimu na taarifa za kidijitali za watoa huduma za fedha.

Mfumo wa wa FSR ni mfumo wa habari za soko la fedha, unaoruhusu mwingiliano wa mfumo mmoja na mwingine na kurahisisha taarifa na takwimu za kifedha kwa urahisi na wenye ufanisi zaidi.

Amesema mfumo huo utaongeza usimamizi na kudhibiti wa masuala ya fedha na kupunguza matukio ya kiuhalifu yanayoweza kutokea.

Amesema mfumo huo ni wa takwimu za wazi na utasaidia kudhibiti wizi na upotevu wa fedha, kwani mtu akiingia katika mfumo huo, atakuwa akionekana na shughuli anayoifanya.