Zaidi ya shilingi Milioni 154 zimetumika kujenga vyumba vitatu vya madarasa na kukarabati shule ya Msingi Luagala ‘B’ Wilayani TandahimbaAkizindua madarasa hayo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba amesema madarasa hayo yamewekwa na madawati tayari kwa wanafunzi kuendelea na masomo“Tumezindua madarasa haya lakini pia wametukabidhi shule ikiwa katika muonekano unaovutia ambapo kazi hii imefanywa na taasisi ya Eclat na Upendo ,”amesema Waryuba
Naye Mwenyekiti wa taasisi ya Eclat Toima Kiroya ameeleza kuwa katika mradi huo wameweza kujenga vyumba vitatu vya madarasa,kukarabati majengo 8,kisima chenye ujazo wa Lita 150,000,matundu 16 ya Choo,madawati 65,meza za walimu 16 na viti 16
Hata hivyo Dk Fred Heimbach wa Upendo Society kutoka Ujerumani ameeleza kuwa madhumuni ya ushirika huo ni kuboresha miundo mbinu katika sekta ya elimu
Sambamba na Hilo Meneja wa mradi huo Msham Bashir ameishukuru serikali kwa kushirikiana kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Wilaya hivyo wananchi wanajukumu lankutunza miundo mbinu hiyo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba akizindua madarasa hayo akiwa na wafadhili waliowezesha mradi huo
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba na Mwenyekiti wa Eclat wakisaini makabidhino hayo
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sebastian Waryuba akikabidhi hati ya makabidhino Afisa Elimu Msingi Wilaya Hadija Mwinuka
Matundu ya Choo kwa ajili ya wanafunzi na walimu Wao
Meneja wa mradi Msham Bashir (mzawa qa Luagala)ambaye ndiye aliwashawishi kuja kuboresha miundombinu ya Elimu Wilayani hapo
Shule ya msingi Luagala ‘B’ katika muonekano mpya
Wananchi wa Kijiji Cha Luagala ‘B’wakishuhudia uzinduzi wa shule