**********************
NA EMMANUEL MBATILO
Aliekuwa Katibu Mkuu wa baraza la Vijana taifa BAVICHA, Bw.Julius Simbeye ameamua kuachana na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo na kutokuweka wazi atahamia chama gani.
Akizungumza na Wanahabari Bw.Simbeye amesema kuwa kila chama Duniani kina malengo na madhumuni yake na lengo kubwa la chama ni kuchukua dola hivyo ni tofauti na chama cha CHADEMA.
“Chadema kimetoka kuwa chama cha kuchukua dola na sasa kimekuwa kikundi cha watu wachache ambacho kinaendeshwa kitaasisi binafsi na sio kama chama”. Amesema Simbeye.
Amesema kuwa Chadema haipo imara tunadanganyana wameamua kukitoa Chama kwenye malengo ya msingi na kuwa taasisi ya mtu binafsi na bado wanaendelea kuwaaminisha watanzania kuwa chama kipo imara muda wote jambo ambalo si kweli.
“Ninaamua kwa makusudi kujivua uwanachama wa CHADEMA na nitapumzika siasa kwa muda ili niweze kupata nafasi ya kufikilia ni chama gani kina malengo ya dhati kuchukua dola na kujiunga nacho”. Amesema Simbeye.