Mlowa Mkoani Songwe ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha akieleza namna Serikali inavyowawezesha wananchi kuondokana na vitendo vya ukatili wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipokuwa Mkoani hapo.
Msanii Shetta na G nako wakitumbuiza eneo la Mlowa Mbozi mkoani Songwe wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipokuwa mkoani hapo.
Baadhi ya wananchi wa Mlowa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wakifuatilia msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia ulipokuwa Mkoani hapo.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu Songwe
Uwepo wa kipato katika familia hasa mwanamke akiwezeshwa kiuchumi kunachangia kupunguza kuwepo kwa vitendo vya ukatili katika jamii zetu.
Hayo yamebainishwa Mlowa Mkoani Songwe na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Imelda Kamugisha wakati msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia uliposimama Mkoani hapo.
Amesema kuwa Serikali katika kupambana na vitendo vya ukatili imeanzisha mpango mkakati wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto uliziozinduliwa mwaka 2017/2018 na kumalizika mwaka 2021/2022.
“Serikali inawezesha wananchi kiuchumi hasa wanawake katika Halmashauri zetu na taasisi za fedha wananchi tuchangamkie fursa hii” amesema
Bi. Imelda amewasihi wanaume kuwapa ushirikiano wanawake katika kuhakikisha wanaweza kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili waweze kuchangia maendeleo ya familia jamii na Taifa.
Akizungumzia masuala ya Kisheria Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Happy Msimbe amesema Serikali inasimamia Sheria mbalimbali katika kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwepo Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inayomlinda mtoto.
“Sheria zinasimamiwa ipasavyo nitoe wito kwa wananchi kutoa taarifa za vitendo vya ukatili vinavyotokea katika jamii zetu” alisema.
Ameongeza kuwa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inapewa nguvu na Sheria nyingine inayosaidia kuwezesha watoto kupata haki zao za msingi zitakazosaidia kuboresha ustawi wao.