Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa kati kati akizungumza na wananchi wa kata ya Nia njema hawapo pichani katika mkutano wa hadhara ambao aliuandaa kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto za wananchi hao.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Baadhi ya wazee wa Kata ya Nia njema Wilayani Bagamoyo wakiwa wanasikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo katika mkutano huo wa hadhara ambao ulihudhuliwa na wadau mbali mbali wa maendeleo pamoja na viongozi wa serikalia na wakuu wa Idara.(PICHA NA VICTOR MASANGU.)
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Kulia Zainabu Kawawa akiwa anasikiliza moja na hoja ambazo zilikuwa zinatolewa na wananchi wa kata ya Nia njewa wakati wa mkutano huo amabao ulifanyika katika viwanja vya shule ya msingi nia njema.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Diwani wa Kata ya Nianjema Abdul Pyalla akizungumza jambo na wananchi katika Mkutano wa adhara ambao uliandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi kero zao ili kuweza kuzitafutia ufumbufu.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mkuu wa kituo cha Polisi Bagamoyo Michael Kakoshi licha ya kulinda hali ya usalama katika eneo hilo la mkutano wa adhara akiwa anasikiliza changamoto mbali mbali ambazo zilikuwa zikitolewa na wananchi wa kata hiyo ya nia njema.(PICHA NA VICTOR MASANGU).
******************************
NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
BAADHI ya wazee wanaoishi katika kaya masikini na mazingira magumu Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani wameiomba serikali ya awamu ya tano kuingilia kati sakata la kero yao kubwa ya kuonewa kwa kipindi kirefu kutokana na kutopatiwa fedha ambazo zinatolewa na mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) kwa ajili ya kujikimu kimaisha pamoja na kuanzisha miradi midogo midogo.
Hayo yalibainisha wakati wa mkutano wa adhara aambao umeandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bgamoyo Zainabu Kawawa kwa wananachi wa Kata ya nia Njema kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili ili kuzitafuatia ufumbuzi pamoja na kuweka mikakati ya kuleta maendeleo kwa wananchi kwa ushirikiano wa serikali na jamii kwa ujumla.
Aidha mmoja wa wazee hao wakizungumza kwa niaba ya wezake wanaoishi katika kaya masikini Ole Shamba alisema kwamba wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa katika suala zima la upatikanaji wa fedha kutoka Tafas hivyo wanajikuta maisha yao yanakuwa ni magumu kutokana na kukosa mahitaji muhimu wao na familia zao.
“Kwa kweli huu mpango kiukweli unatusumbua sana na leo hii kwa kuwa amekuja Mkuu wetu wa Wilaya Zainabu Kawawa tumeona ni bora tuseme kilio chetu ambacho kimekuwa ni kero kubwa ya siku nyingi maana hata sasa nimesahau kutokana na kipindi kimekuwa ni kirefu sana na ukizingatia taratibu zote tumeshazikamilisha sasa nashindwa kuelewa kwa hiyo tunaomba sana serikali yetu itusaidia katika suala hili,”aslisema Shamba.
Aidha katika hatua nyingine wazee hao walimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kuwa na utaratibu wa kufanya mikutano na wananchi wake kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili na kumuomba alichukulia ssuala hilo kwa uzito mkubwa ili fedha zote ambazo zinatolewa ziweze kuwafikiwa walengwa na sio vinginevyo.
Kwa upande wake MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa baada ya kusikiliza kilio hicho ameahidi kulivalia njuga suala hilo na kuwaagiza watendaji wa TASAF kuhakikisha fedha zote zinazotolewa zinawafikiwa walengwa kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa bila ya ubaguzi na upendeleo na kuachana kabisa na vitendo vya ya kufanya ubadhilifu kwa maslahi yao binafsi kwani atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Pia ,Mkuu huyo alibainisha kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawaletea wananchi maendeleo kupitia miradi mbali mbvali na mifuko ambayo imeanzishwa hivyo atahakikisha kwamba wale walengwa wote ambao wanaishi katika mazingira magumu pamoja na kaya ambazo ni masikini wanakwekwa katika utaratibu wa kusaidiwa fedha kwa kuzingatai vigezo mbali mbali ambavyo vimetolewa na Tasaf.
“Kwa kweli katika hili jambo mimi nitalisimamia kweli kweli kwa kushirikiana na viongozi wangu wengine pamoja na watendaji wa mamlaka husika lakini kikubwa fedha hizi ni lazima ziwafikie watu ambao ni walengwa na wanaoishi katika kaya masikini, na kitu kingine watendaji inabidi kuchungua uhalisia wa kaya husika kama ni masikini au lah na wananchi msiwe wadanganyifu ili wananchi wa maeneo husika waweze kupata haki zao, awe bibi au babu sio anakaa Mkuranga unamwandikisha bagamoyo hii hapana,”alisema Zaibu.
Kwa upande wake Mratibu wa ….TASAF Wilaya ya Bagamoyo Dionise Mahilane amesema kwamba kwa sasa wamejipanga kuondokana na changamato ya kuwepo kwa baadhi ya wananchi kuwa wadanganyifu katika utoaji wa taarifa zao ili kuhakikisha inawasaidia wale ambao ni walengwa na wanaishi katika kaya masikini kwa kuzingatia vigezo vilivyoweka sambamba na kutoa elimu jumuishi kwa jamii.
Naye Diwani wa Kata ya Nianjema Abdul Pyalla alisema kuwa kwa sasa kutokana na kuwepo kwa changamoto ya baadhi ya kaya masikini kutokupata fedha hizo watafanya zoezi la kupita katika mitaa ili kutoa elimu ya watu ambao wanastahili kusaidia sambamba na kuhakiki orodha ya kaya ambazo zinatakiwa kupatiwa msaada lengo ikiwa ni kuondokana na kero hiyo ambayo imekuwa ni usumbufu mkubwa.