Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, akizungumza wakati wa akifungua Mkutano wa Wataalamu wa Masuala ya Nishati kwa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC) uliofanyika Jijijni Dar Es Salaam kuanzia februari 25 hadi 28, 2020
Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni Kamishna wa Mafuta na Gesi kutoka Wizara ya Nishati wa Tanzania, Adam Zuberi akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Wataalamu wa Masuala ya Nishati kwa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC)uliofanyika Jijijni Dar Es Salaam kuanzia februari 25 hadi 28, 2020.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, (katikati) waliokaa, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Wataalamu wa Masuala ya Nishati kwa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC)uliofanyika Jijijni Dar Es Salaam kuanzia februari 25 hadi 28, 2020 baada ya kufungua mkutano huo.
Washiriki mkutano wa Wataalamu wa Masuala ya Nishati kwa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC)uliofanyika Jijijni Dar Es Salaam kuanzia Februari 25 hadi 28, 2020 wakimsikiliza katibu mkuu wa wizara ya Nishati, Zena Said( hayupo pichani) wakati akifungua mkutano huo.
Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said( wapili kulia), Mwenyekiti wa mkutano wa Wataalamu wa Masuala ya Nishati kwa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC) ambaye pia ni Kamishna wa Mafuta na Gesi wa Wizara ya Nishati, Adam Zuber,( wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa masuala ya miundombinu wa SADC( wa pili kulia) wakifuatilia majadiliano katika mkutano huo uliofanyika Jijijni Dar Es Salaam kuanzia Februari 25 hadi 28, 2020.
Kaimu kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala, Edward Ishengoma( CERE)( katikati), na Kamishna Msaidizi wa Umeme,( ACE) Mhandisi Innocent Luoga( wa pili kushoto) wakifuatilia majadiliano katika mkutano wa Wataalamu wa Masuala ya Nishati kwa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC) uliofanyika Jijijni Dar Es Salaam kuanzia Februari 25 hadi 28, 2020.
Kamishna Msaidizi Maendeleo ya umeme, Mhandisi Styden Rwebangila (katikati) wakifuatilia majadiliano katika mkutano wa Wataalamu wa Masuala ya Nishati kwa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC) uliofanyika Jijijni Dar Es Salaam kuanzia Februari 25 hadi 28, 2020.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Wataalamu wa Masuala ya Nishati kwa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC) ambaye ni Kamishna msaidizi wa Maendeleo ya umeme( ACED) wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Styden Rwebangila( kulia) na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya maudhui ya mkutano huo, Emilian Nyanda( katikati) wakibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Umahiri cha Uendelezaji wa Nishati Jadidifu na Matumizi bora ya Nishati kutoka nchini Namibia, Kudakwashe Ndhlukula .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, na Mkurugenzi wa masuala ya Miundombinu wa SADC,Mapalao Rosemary Makoena wakiteta jambo wakati wa Mkutano wa Wataalamu wa Masuala ya Nishati kwa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC) uliofanyika Jijijni Dar Es Salaam kuanzia Februari 25 hadi 28, 2020.
Mkurugenzi wa SHIRIKA LA umeme Tanzania( TANESCO),dkt. TITO Mwinuka( tatu kushoto) akifuatilia mada katika Mkutano wa Wataalamu wa Masuala ya Nishati kwa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC) uliofanyika Jijijni Dar Es Salaam kuanzia Februari 25 hadi 28, 2020.
………………………………………………………………………………………………………….
Na Zuena Msuya, Dar es salaam,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, amesema Mkutano wa Wataalamu wa Masuala ya Nishati kwa Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC) unalenga kuanzisha mtandao wa upatikaji umeme wa uhakika, wakutosha na unaopatikana kwa gharama nafuu ili kuchochea ukuaji wa uchumi na viwanda katika jumuiya hiyo.
Zena alisema hayo, mara baada ya kufungua mkutano wa siku nne ulioanza leo, Februari 25 hadi 28, 2020, Jijini Dar Es Salaam, uliwakutanisha Watalaamu na Makamishina wa Nishati kutoka nchi 12 wanachama wa SADC ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa uamuzi uliopitishwa na Wakuu wa nchi wanachama wa jumuia hiyo pamoja na Mawaziri wanaohusika na masuala ya nishati katika nchi hizo.
Alisema kwa mujibu wa taarifa zilizopo, mahitaji ya umeme kwa nchi za ukanda huo yanatarajiwa kuongezeka kutoka kiwango cha Terawatt 300 hadi Terawatt 580 kwa saa ifikapo mwaka 2030 sawa na ongezeko la mahitaji ya Megawati Milioni 280 kwa saa.
Aidha alisema kuwa, vyanzo vya nishati vilivyopo kwa sasa katika nchi za SADC, vinaweza kuzalisha nishati kwa kutumia Joto Ardhi Megawati 15,000, Upepo Megawati 110,000, Maji Megawati 350,000 na Jua Megawati Milioni 10.
Zena aliongeza kwa kusema kuwa, pamoja na utajiri wa vyanzo vya nishati barani Afrika, nchi nyingi za Jumuiya hiyo bado zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa nishati ya kutosha.
Aliweka wazi kuwa, katika mkutano huo sasa, wataalamu hao watajadili na kuhakikisha kuwa nchi zitakazozalisha nishati kwa wingi na endelevu inayokidhi mahitaji ya matumizi ya ndani na ziada, inawauzia wengine kama biashara nyingine zinavyofanyika
Aidha pia kuna kiwango kikubwa sana cha ugunduzi wa Gesi katika nchi kadhaa ikiwamo Tanzania na Msumbiji.
“Mahitaji ya mafuta na gesi pia yataongezeka, katika sekta zote ikiwamo viwanda, usafiri, taasisi na makazi katika ukanda huo, wakati mahitaji yakitarajiwa kuongezeka, inasikitisha kuona asilimia 5% tu ya watu vijijini katika jumuia hiyo ndiyo wanapata huduma za umeme,” amesema Zena wakati akifungua mkutano huo,
Zena alisema kuwa uhamasishaji wa matumizi ya nishati mbadala kwa matumizi ya kupikia imekuwa changamoto kutokana na uhaba wa nishati yewenyewe.
“Huwezi kumwambia mwananchi asitumie mkaa wakati hakuna mbadala wa kutumia, sasa tunaelekea kuzalisha umeme mwingi na gharama nafuu, itasaidia kupunguza matumizi ya nishati ya mkaa na hatimaye mabadiliko ya tabia yanayotuletea majanga mbalimbali kama vile mafuriko yataondoka,” alisema Zena.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mkutano huo ambaye pia ni Kamishna wa Mafuta na Gesi kutoka Wizara ya Nishati wa Tanzania, Adam Zuber alisema, kuwa hoja zitakazojadiliwa katika Mkutano huo ni pamoja na uanzishaji wa Kituo cha Umahiri cha Kuendeleza Nishati Jadidifu na Matumizi bora ya Nishati kwa Nchi za jumuia hiyo, mapitio ya Itifaki ya Nishati ya 1996 pamoja na utekelezaji wa Mpango Kabambe wa utekelezaji wa Matumizi bora ya Gesi asilia katika nchi za SADC.
Pia kutakuwa na mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Sekta ya Nishati chini ya Mpango Kabambe wa Maendeleo ya Miundombinu katika Mtangamano(RIDMP), utakaokoma 2027.
“Kwa hiyo mkutano huu ni muhimu sana kwa nchi zetu kwani wataalam hawa watatoa muelekeo chanya ya kupatikana kwa umeme wa uhakika katika nchi wanachama wa SADC ambayo yatawasilishwa katika ngazi za Mawaziri ili na wao kutoa maamuzi”, alisisitiza Zuberi.
Zuberi alisema kuwa baada ya kukamilika kwa mkutano huo, kamati husika itaandaa ripoti itakayowasilishwa na baadaye kujadiliwa katika baraza la mawaziri wa masuala ya Nishati itakapofika mwezi Mei, mwaka huu.
Ikumbukwe kwamba , Mkutano wa 39 wa jumuiya hiyo uliofanyika Agosti 17 na 18,2019, jijini Dar Es SALAAM na kukabidhi majukumu ya uongozi wa jumuiya hiyo kwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya Rais wa Namibia, Hage Geingob kumaliza muda wake.
Baada ya tukio hilo, Tanzania ilianza kuratibu na kusimamia vikao mbalimbali vya kamati za watalaamu kutoka sekta mbalimbali vikao hivyo vinaendelea na baadaye katika ngazi ya mawaziri wan chi wanachama.