……………………………………………………………………………………………………
Vinara wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara klabu ya Simba imefanikiwa kutinga hatua ya
robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation CUP baada ya kuichapa 3-2 kwa njia ya matuta Stand United Mchezo uliochezwa uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Simba walipata bao la kwanza kupitia mkwaju wa penalt lililofungwa na Hassan Dilunga katika dakika ya 60 hata hivyo Stand United walisawazisha bao hilo kupitia kwa mshambualiaji wake Miraji Salehe
Hadi dakika 90 za Mwamuzi kumalizika timu zote zilikuwa zimefungana bao 1-1 hivyo kulazimika kuingia hatau ya mikwaju ya Penalti na Simba kuibuka na ushindi huo.
Shujaa wa Simba ni Kiungo mshambuliaji Hassan Dilunga aliyefunga bao katika 90 na pia alimalizia kupiga Penalti ya mwisho ambayo imewapeleka robo Fainali wengine waliofunga Penalti ni Clatous Chama na Deo Kanda huku Ibrahimu Ajibu na Meddie Kagere wakikosa Penalti.
Kwa upande wa Stand United waliokosa penalt walikuwa wachezaji watatu akiwemo Miraji Salehe na Maulid Fadhil
Timu nyingine ambazo zimeingia hatua ya robo katika fainali hiyo ni timu Namungo FC, Ndanda FC pamoja na Sahare All Stars.
Michuano hiyo inatarajia kuendelea kesho katika viwanja mbalimbali hapa nchini ila macho na masikio yatakuwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Yanga watawakaribisha matajiri wapya toka Daraja la kwanza Gwambina FC.