Mbunge wa bunge hilo George Odongo akiongea na wanahabari nje ya bunge.
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Wabunge wa bunge la Afrika mashariki wameibua tena mjadala wa tatizo la ukosefu wa fedha za kutosha kutekeleza majukumu ya kila siku ya jumuiya na kuliomba Baraza la mawaziri kuona uwezekano wa kulipatia ufumbuzi wa kudumu tatizo hilo.
Akiongea wakati akichangia mjadala wa ripoti ya ukaguzi fedha hilo Mbunge wa EALA Mariamu Ussi alisema kuwa suala hilo ni changamoto ambayo inahitaji kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Alieleza kuwa Kuna haja ya sheria kutumika kutekeleza baadhi ya majukumu ili kuondoa suala hilo kuweza kuifanya jumuiya hiyo kuweza kusonga mbele katika kutekeleza shughuli zake za kila siku.
“Sasa ifike mahali Baraza la mawaziri kufanya juhudi za maksudi kuweza kupata suluhisho la kudumu la ukosefu wa fedha za kutosha kutekeleza majukumu ya kila siku”
Kwa Upande wake Mbunge wa bunge hilo Mhandisi Suzan Masay alisema kuwa suala hilo linatakiwa kujadiliwa kwa kina na Baraza la mawaziri na kuja na suluhisho la kudumu kuweza kuondoa changamoto ya kutokuwa na fedha za kuendesha jumuiya hiyo.
Alisema kuwa suala kutumia sheria ili lengo ifikiwe kwa kuwa suala hilo limekuwa likiendelea kuibuka Mara kwa Mara kwa kuonyesha kasi yake ya kutatua bado inasuasua.
“Baraza letu la mawaziri linahitaji kukaa chini kuja na dawa thabiti ya kutatua changamoto ya uhaba wa kifedha za utekelezaji wa majukumu ya jumuiya japo suala la matumizi limeonekana kwenda vizuri kwa sasa baada ya bunge kuwa wakali kwenye ripoti zilizopita”.
Nae mbunge wa bunge hilo George Odongo alisema kuwa mjadala huo unaohitajika kufanyiwa kazi kwa haraka kuondoa sintofahamu hiyo ambayo imeonyesha kuwepo kwa uhaba wa utekelezaji wa shughuli za jumuiya hiyo.