Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi ( wa kwanza kulia) akizungumza leo na ujumbe wa Benki ya Dunia (WB) kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika ripoti ya utafiti juu ya usikilizaji na umalizaji wa mashauri ya jinai kwa wakati. Wa pili kulia ni Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sirwatt na wengine ni baadhi ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania.
Aidha Jaji Kiongozi aliueleza ujumbe huo kuhusu mabadiliko ya sheria mbalimbali yalivyowezesha usikilizaji wa mashauri ya jinai kwa haraka. Ujumbe huo uko nchini kwa ziara ya kikazi.
Ujumbe wa Benki ya Dunia (WB) na baadhi ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania wakimsikiliza Jaji Kiongozi (ambaye hayupo pichani).
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi ( wa kwanza kulia) akifafanua jambo leo kwa ujumbe wa Benki ya Dunia (WB) kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika ripoti ya utafiti juu ya usikilizaji na umalizaji wa mashauri ya jinai kwa wakati. Wa pili kulia ni Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sirwatt na wengine ni baadhi ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania.
Mtaalamu wa Benki ya Dunia (WB), Bw. Waleed Malik (wa pili kushoto) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo.
Mtaalamu wa Benki ya Dunia (WB), Bi. Debohar Isser (wa kwanza kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo, ( wa tatu kushoto) ni Bi. Clara Maghani na (wa nne kushoto) ni Bw. Denis Biseko (wote ni wataalamu kutoka WB).
(Picha na Magreth Kinabo – Mahakama ya Tanzania)