katibu Mkuu wizara ya maliasaili na utalii, Profesa Adolph Mkenda, na waandishi wa habari mara baada ya kupokea ugeni wa Waziri wa Maendeleo ya Ushirikiano wa Kimataifa na Biashara kutoka Finland Ville Skinnari kikao hicho kimefanyika Mtumba jijini Dodoma.
Sehemu ya ugeni wa Waziri wa Maendeleo ya Ushirikiano wa Kimataifa na Biashara kutoka Finland Ville Skinnari umkimsikiliza katibu Mkuu wizara ya maliasaili na utalii, Profesa Adolph Mkenda (hayupo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari na ugeni huo leo jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Biashara, Mhe Ville Skinnari,akizungumza kwenye kikao cha pamoja kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Adolf Mkenda chenye lengo la kukubaliana kushirikiana katika kukuza sekta ya Utalii nchini kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma.
Balozi wa Finland nchini, Riita Swan,akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Adolf Mkenda mara baada ya kuingia makubaliano ya kukuza sekta ya Utalii nchini kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Ushirikiano wa Kimataifa na Biashara kutoka Finland,Ville Skinnari
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuingia makubaliano ya kukuza ushirikiano katika Sekta ya Utalii nchini na nchi ya Finland kushoto kwake ni Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Biashara kutoka Finland, Ville Skinnari.
Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Biashara kutoka Finland, Ville Skinnari,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuingia makubaliano ya kukuza ushirikiano katika Sekta ya Utalii nchini na nchi ya Tanzania kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Adolf Mkenda
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
……………………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Tanzania na Finland zimekubaliana kushirikiana katika kukuza sekta ya utalii nchini pamoja na sekta zingine za kimaendeleo lengo likiwa ni kuinua uchumi wa Nchi.
Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dodoma wakati wa kikao cha pamoja kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Adolf Mkenda na Waziri wa Maendeleo ya Ushirikiano wa Kimataifa na Biashara kutoka Finland Ville Skinnari.
Akizungumza baada ya mazungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Balozi wa Finland nchini, Riita Swan, Katibu Mkuu Prof Mkenda amesema serikali imeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kutoka nje ya Nchi kuja kuwekeza na kufanya biashara.
Amesema katika mazungumzo hayo yalijikita katika kuzungumzia manufaa ya misitu na namna ambavyo wataweza kumaliza changamoto ya uchomaji misitu na kuhamasisha upandaji miti.
” Tunawashukuru wenzetu wa Finland ambao kwa hakika tumekua tukishirikiana kwa muda mrefu, tumejadili kwa pamoja umuhimu wa kuendeleza nishati mbadala ili kuepuka matumizi ya mkaa ambayo husabahisha uchomaji wa misitu.
Lakini wao pia wametuahidi kutusaidia katika uwekezaji wa viwanda vinavyozalisha bidhaa zitokanazo na misitu kwani wao wamekua ni wabobezi kwenye eneo hilo,” Amesema Prof Mkenda.
Profesa, Adolph Mkenda amesema kuwa serikali imeewaalika wawekezaji hao kutokana na uzoefu wa nchi hiyo katika sekta ya misitu.
“ Tumewaalika walete wawekezaji katika eneo la viwanda vya mazao ya misitu kutoka Finland, kwasababu katika eneo hiki wanautalaamua mzuri sana.”
” Tumemualika pia Mhe Waziri kuja kutembelea vivutio vilivyopo nchini kwetu ili awe Balozi mzuri wa kututangaza na kuhakikisha tunanufaika na wingi wa watalii wanaotoka Finland.
Pia tumewaalika kuja kuwekeza kwenye sekta ya utalii nchini kwetu hasa katika eneo la Hoteli na tumewahakikishia kwamba mazingira ni salama na tutawapa ushirikiano wote,” Amesema Prof Mkenda.
Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Ushirikiano wa Kimataifa na Biashara kutoka Finland, Skinnari amesema kuwa Tanzania na Finland zimekuwa na ushirikiano wa taribani miaka 50 katika nyanja mbalimbali na kuwa kwa sasa wanaangalia namna ya kuzidi kuimarisha ushirikiano kwa miaka mingi ijayo.
Skinnari alitumia fursa hiyo kupongeza juhudi za serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuwa kwa kufanyia hivyo ni muhimu kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla na kusisitiza kuwa na mabadiliko chanya na ndio maana suala la uhifadhi endelevu wa misitu ni kipaumbele.
Amesema kuwa kwa upande wa viwanda, nchi yake imepiga hatua hususani katika sekta ya misitu, tekinolojia ya habari(ICT) na kusisitiza kuwa ndio baadhi ya mambo ambayo wamelenga kushirikiana na Tanzania.
” Tumewaeleza wenzetu kwamba suala la utunzaji wa mazingira hasa kulinda misitu yetu ni muhimu sana, tumewaahidi tutashirikiana katika kuanzisha viwanda vinavyozalisha bidhaa zitokanazo na misitu ili kuongeza pia fursa ya ajira na kukuza uchumi wa Nchi,” Amesema Skinnari.