……………………………………………………………………………………………………………
Na Magreth Mbinga
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda amewataka mkuu wa wilaya ya Ilala na Mkurugenzi wake kuanza ujenzi wa barabara kwa haraka siku ya kesho .
Amezungumza hayo leo katika mkutano wa bodi ya barabara ambao ulihusisha kamati tano ambazo zilienda kufanya tathimini na kuleta changamoto na ushauri nini kifanyike ili kuweza kufanya ukarabati wa barabara hizo.
Pia amesema Kuna jumla ya kilometa 5153 ikiwa na mchanganuo wa Km 1300 kiwango cha lami,Km 1170 changalawe na Km 2979 ya udongo.
Makonda amesema serikali imetenga Billioni 165 kwa ajili ya ukarabati wa barabara fedha ambazo zimetengwa kwa makundi billioni 23 kwa ajili ya TARURA ,Billioni 29 kwaajili ya UDART na Billioni 113 kwa ajili ya TANROADS
Vilevile Makonda amesema kuwa wilaya ya Kigamboni hawakupata Fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mitaa lakini ameipongeza wilaya hiyo kwa kujenga barabara.
“Ninaitaka mamlaka husika na viongozi wa mitaa na madiwani kufanya kazi ipasavyo kwa kuhakikisha wanasimamia usafi ili watu wasichafue mazingira kwa kutupa taka barabarani, kwenye mifereji na mito ili kuepusha mafuriko yasitokee”.Alisema Makonda.