Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imemuachia huru mwandishi wa Habari za Uchunguzi Erick Kabendera, huku ikimtaka kulipa faini kwa makosa yake yote mawili ikiwemo utakatishaji fedha na kukwepa kulipa kodi, hii ni baada ya kuondolewa shtaka la Kuongoza genge la Uhalifu.
Katika hukumu iliyosomwa na Hakimu Janeth Mtega imemtaka mtuhumiwa Erick Kabendera kulipa kiasi cha pesa za kitanzania shilingi laki mbili na elfu Hamsini (250,000) au kutumikia kifungo cha Miezi mitatu jela. Adhabu hiyo inaambatanana fidia ya Shilingi za kitanzania Milioni 172, hii ni kwa kosa la kushindwa kulipa kodi.
Kosa la pili limemtaka Erick Kabendera kulipa faini ya shilingi za kitanzania Milioni mia Moja (Mil 100) hii ikiwa ni adhabu kwa kosa la Utakatishaji fedha katika kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili.