Katibu Mkuu wa CCM,Dk Bashiru Ally,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akiwapokea madiwani 11 wa Chma cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa Jiji la Mbeya wakiongozwa na Meya wa Jiji hilo David Mwashilindi na katibu
wa wilaya ambao wametangaza rasmi kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) hili ni pigo kwa Mhe.Sugu
Sehemu ya Madiwani 11 wa Chma cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa Jiji la Mbeya wakiongozwa na Meya wa Jiji hilo David Mwashilindi na katibu
wa wilaya ambao wametangaza rasmi kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) hili ni pigo kwa Mhe.Sugu
……………………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
MADIWANI 11 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa jiji
la Mbeya wakiongozwa na Meya wa Jiji hilo David Mwashilindi na katibu
wa Wilaya wametangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Katibu Mkuu wa CCM,
Dk Bashiru Ally wakati wa kuwapokea amesema kuwa haya ni mafuriko kwa kupokea viongozi wengi wa upinzani kwa wakati moja na wamekuja kukiongezea nguvu na
uwezo Chama chetu.
Madiwani hao ambao kata wanazoongoza ziko kwenye mabano ni Fabian
Sanga (Ghana), Fanuel Kyanula (Sinde) ambaye pia ni Naibu Meya,
Davidi Mwashilindi (Nzouwa) ambaye ni Meya, Anyandwile Mwaluhubh
(Isanga), Kigenda Kasebwa (Ilomba Viti Maalum) na Dickson Mwakilasa
(Ilomba).
Wengine ni Costantine Mwakyoma (kalobe) Furaha Mwandalim (Ilemi) Henry
Mwangambaku (Forest) ambaye pia ni katibu wa Wilaya, Anderson Ngao
(Mwasanga) na Ibrahim Mwampwani (Isyesye)
Halmashaur ya Jiji la Mbeya inaongozwa na Mbunge wa Chadema, Joseph Mbilinyi.
Dk Bashiru amesema kuwa hii si mara ya kwanza kupokea madiwani na meya.
“Tulishawahi kufanya hivyo Ilala na katika jiji la Arusha tulipokea madiwani pamoja na Meya hivyo ni mwendelezo tu wakukiongeza nguvu chama chetu ili kuendelee kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo bora”amesema Bashiru
Aidha Dk.Bashiru amesema kuwa wapo wanachama wa upinzani wasio na vyeo wanaendelea kujiunga na CCM ni kazi ya kupokea wanachama wapya.
“Kurudi kwa madiwani 11 si jambo la kubeza kwetu sisi ni kuongeza
nguvu na hii ni dalili nzuri kwa CCM kulichukua jimbo hili” amesisitiza
Kwa upande wake, aliyekuwa meya wa jiji la Mbeya, Mwashilindi amesema
sasa sio mwana chadema tena na amerudi kwenye chama chake chenye kuwajali wananchi wanyonge kuwaletea maendeleo bora.
“Nimekuwa meya wa Jiji la Mbeaya kwa miaka minne, nimeona juhudi kubwa
zikifanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John
Magufuli, ni mambo makubwa tunaiona Tanzania mpya, Chadema tulikuwa
hatuna ajenda ya maendeleo, ajenda kubwa ni ugomvi,” amesema