Home Michezo SAMATTA ASHINDWA KUIBEBA ASTON VILLA YACHAPWA MECHI YA TATU MFULULIZO LIGI YA...

SAMATTA ASHINDWA KUIBEBA ASTON VILLA YACHAPWA MECHI YA TATU MFULULIZO LIGI YA ENGLAND

0

MSHAMBULAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amecheza dakika zote 90, timu yake, Aston Villa ikiendelea kuboronga katika Ligi Kuu ya England baada ya kuchapwa mabao 2-0 na wenyeji, Southampton Uwanja wa St. Mary’s, Southampton, Hampshire.
Matokeo hayo ni mabaya kwa kikosi cha Dean Smith, kwani kinabaki nafas ya 17 na pointi zake 25 za mechi 27, kikiwazidi pointi moja moja, wote West Ham United na Watford wanaofuatia mbele ya Norwich City wanaoshika mkia wakiwa na pointi 18 za mechi 26.
Mabao yaliyoizamisha Aston Villa leo yamefungwa na Shane Long dakika ya nane na Stuart Armstrong dakika ya 90 

Kocha Dean Smith amesema kwamba kila mechi kwao ni fainali, lakini leo wamecheza ovyo mno na kama watacheza hivyo pia wikiendi ijayo, Manchester City watatwaa taji la tano la Kombe la Ligi England ndani ya miaka saba.
Huo unakuwa mchezo wa tatu mfululizo wa EPL kwa Samatta tangu ajiunge na Aston Villa Januari akitokea KRC Genk ya Ubelgiji baada ya kucheza pia dhidi ya AFC Bournemouth ugenini na Tottenham Hotspur nyumbani, zote timu yake ikipoteza pia.
Samatta pia alicheza mechi ya marudano ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, Aston Villa ikiichapa Leicester City 2-1 Januari 28 na kutinga fainali ambako sasa itamenyana na Manchester City Machi 1 Uwanja wa Wembley
Kikosi cha Southampton kilikuwa; McCarthy, Ward-Prowse, Stephens, Bednarek, Bertrand, Hojbjerg, Smallbone/Romeu dk80, Armstrong, Djenepo, Long/Adams dk73 na Ings/Obafemi dk73.
Aston Villal; Reina, Konsa/Hourihane dk59, Mings, Hause, Guilbert, Luiz, Nakamba/Baston dk81, Targett, El Ghazi/Trezeguet dk28, Samatta na Grealish.