Home Mchanganyiko WASAFIRISHAJI DAWA ZA KUREVYA WABUNI MBINU MPYA MOROGORO

WASAFIRISHAJI DAWA ZA KUREVYA WABUNI MBINU MPYA MOROGORO

0

Jafari Idd Mshana Mkazi Wa Dar Es Salaam (Wakwanza kulia ) anayetuhumiwa kusafirisha wahamiaji haramu,akiwa na wahamiaji hao Raia wa Ethopia.

.Gari aina ya prado lililotumika kusafirishia dawa za kurevya aina ya Bhangi.

**************************

NA FARIDA SAIDY MOROGORO

Kutokana na msako mkubwa unaofanywa na Jeshi la Polisi nchini waharifu wa makosa mbalimbali wakiwemo wasafirishaji wa dawa za kurevya wamebuni mbinu mpya za kusafirisha wa dawa hizo,ambapo wanatumia Madumu ya lita 20 kama kifungashio cha kubebea dawa hizo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari kaim Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Mugabo Wekwe amesema mbinu hizo zimebuniwa na wasafirishaji wa bhangi pamoja na wale wa wanaosafirisha wahamiaji haramu ambapo wanabandika namba bandia za magari zinazotumika na
mashirika mbalimbali hapa nchini.

 

Aidha Jeshi la Polosi Mkoa wa Morogoro linamshkilia Jafari Idd Mshana Mkazi Wa Dar Es Salaam kwa kosa la kusafirisha wahamiaji haramu watano Raia wa Ethopia ambao wote wamekutwa wakiwa hawana passport za kusafiria.

 

Katika hatua nyingine kaim kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kufichua uharifu na waharifu wa aina zote waliopo katika maeneo yao.