Home Mchanganyiko USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI WASISITIZWA

USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI WASISITIZWA

0
……………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amesisitiza uwepo wa umuhimu wa ushirikishwaji wa Wananchi kwenye shughuli za kimaendeleo za Kiserikali ili kuimarisha dhana nzima ya utawala bora nchini.
Gavana Shilatu ameyasema hayo alipotembelea mradi wa ujenzi wa Zahanati unaondelea Kijiji cha Lembela kata ya Mihambwe ambapo hakufurahishwa na kitendo cha Wananchi kutojumuishwa kwenye kamati mbalimbali za Halmashauri ya Serikali ya Kijiji.
“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli inasisitiza kuwashirikisha Wananchi kwenye shughuli za kimaendeleo ama za Kiserikali lakini hapa nimesikitika kuona hakuna Mwananchi hata mmoja kwenye kamati za Serikali ya Kijiji, hii si sawa. Haiwezekani ujenzi wa miradi mikubwa kama hii ifanyike pasipo ushirikishwaji wa Wananchi.
Hivyo ndani ya siku tatu kuanzia sasa Mwenyekiti wa Kijijj kaa na Mtendaji wa Kijiji muitishe kikao cha dharura cha Halmashauri ya Serikali ya Kijiji muibue ajenda ya kuongeza Wananchi kwenye kamati za Serikali liende kwenye mkutano wa dharura wa Kijiji ili Wananchi wakapendekeze Wajumbe wanaowaona wanafaa kuingia kwenye kamati miongoni mwao, na si kujifungua wenyewe tu. 
Ni lazima tujenge tabia ya kudumisha utawala bora kwa kuhakikisha ushirikishwaji wa Wananchi kwenye kila hatua.” Alisema Gavana Shilatu.
Gavana Shilatu alisisitiza ujenzi ufanyike kama ambavyo BOQ imeeleza na kuwa na usimamizi imara wa ujenzi wa mradi uendane na thamani ya fedha.
Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na Mtendaji kata, Mtendaji Kijiji, Halmashauri Serikali ya Kijiji pamoja na kamati ya ujenzi ya Kijiji.