***********************
Na Silvia Mchuruza,
Bukoba.
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassimu Majaliwa anatarajia kufanya ziara ya siku mbili katika mkoa wa Kagera yenye lengo la kufanya shughuri za chama cha Mapinduzi(CCM) pamoja na Serikali.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mnamo tarehe 19/02/20209, na kuongeza kuwa, Mh Majaliwa anatarajia kuwasili mkoani humo mnamo tarehe 20/02/2020 saa 03:30 asubuhi katika uwanja wa ndege wa Bukoba.
Ameongeza kuwa katika ziara yake ya siku mbili mh Majaliwa atapata taharifa ya mkoa pamoja na kukagua shughuri za Chama Cha Mapinduzi(CCM) ikiwa ni pamoja na kufanya vikao na viongozi wa chama ndani ya Mkoa ikizingatiwa kwamba yeye ndiye mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoani humo.