******************************
Watanzania wameshauriwa kuendekea kutunza, kuthamini na kuviendeleza vivutio vya utalii kwa kufanya maonyesho mbalimbali yatakayohimiza urithi na utamaduni wa Nchi.
Wito huo umetolewa Leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Lwoga wakati akitoa tariifa ya Maadhimisho ya kumbukizi ya vita vya majimaji na Tamasha la Utalii wa Utamaduni litakalofanyika February 22-27 mwaka huu mkoani Songea likiongozwa na kauli mbiu ‘Mchango wa Vita vya Majimaji katika kuendeleza na kurithisha Urithi wa Utamaduni kwa Maendeleo ya Taifa.
“Kupitia tamasha hilo litatoa fursa kwa Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuenzi kutunza,na kuendeleza Urithi asili na Utamaduni kwa ajili ya kizazi cha sasa na vijavyo kwani ni tunu na kioo cha Taifa la Tanzania na unaleta Umoja,Amani na mshikamano wa kitaifa ikiwa ni pamoja na kutambulisha na Taifa”. Amesema Dkt.Lwoga.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha Bi Christina Ngereza amesema kutakuwa na shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa Elimu Mashuleni,kutakuwa na Maonyesho ya Wajasruamali na taasisi mbalimbali,kutembelea makaburi mawili yaliyopo Makumbusho ya Majimaji ya Mashujaa wapatao 67 walionyongwa na Wajermani na kuzikwa Mjini Songea
“Tamasha hilo litasaidia kuwaelimisha wananchi namna ya kutunza na kuendeleleza vitu vilivyoachwa kama kumbukizi kwa vizazi vijavyo”. Amesema Bi.Christina.