Zoezi la kuruhusu maji kupita kwenye mkondo wake wa asili kwenye bwawa la Mtera linaendelea na hii ni kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea kina cha maji kuongezeka na hivyo kulazimu ziada inayoendelea kuingia ipite kwa njia ya milango mahususi ya kuhamisha maji toka upande wa bwawa kwenda upande wa chini ya bwawa.
Zoezi linashirikisha wataalamu mbalimbali wakiwemo kutoka TANESCO, Bonde la Mto Rufiji na Wizara ya Maji.
Aidha, zoezi hili hili litakuwa endelevu wakati wote ili kuhakikisha maji yanayostahili yanahifadhiwa kwa usalama wa bwawa na miundombinu yake.
Zoezi hili lilianza jana Februari 15, 2020.