************************
Na Woinde Shizza, Arusha
Wanachama Wa chama cha mapinduzi nchini wametakiwa kuondoa tofauti zao na kuvunja makundi haswa katika kipindi hichi wanapoelekea katika uchaguzi Mkuu ili kukiwezesha chama hicho kupita kwa kishindo.
Hayo yamebainishwa na mjumbe Wa kamati kuu CCM Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi Edmund mundolwa alipokuwa akiongea na viongozi Wa chama hicho mkoani Arusha Jana (Leo)kabla ya kuanza ziara ya siku tano ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na chama hicho kupitia ilani
Alisema alisema kuwa katika kuelekea katika uchaguzi Mkuu Wa mwaka huu ni vyema wanachama na viongozi Wa Ccm kuacha makundi ya vyama Mara moja na iwapo kama kunaambao wamegombana ni vyema wapatane na waungane katika kukiletea chama cha mapinduzi ushindi katika uchaguzi ujao Wa Rais ,wabunge na madiwani.
“Mwaka huu tutajitaidi kuleta majina matatu maana majina matatu ni rahisi kuvunja kuliko kuwa na makundi mengi ambayo ayana maana na ambayo yatatuletea makundi ,makundi matatu ni rahisi sana kuziniti kuliko kuwa na mandi mengi yatakayo tuchanganya” alibainisha mundolwa.
Alisema kuwa wanaitaji viongozi Wazuri ambao ,ambao rais atakapo ingia madarakani katika kipindi cha awamu ya pili ,aweze kupata kupata viongozi Waziri Wa kuongeza serikali ,Hulu akibainisha kuwa Rais anataka viongozi wabovu waenguliwe tangu chini wasisubiri mpaka wakakatwe katika ngazi za huu Bali wawashulikiw mapema.
Alisema kuwa mradi huu Wa ufugaji wa Nyuki utasaidia kuwatoa vijana kwenye vijiwe na utawapeleka kwenye uzalishaji ,pia watatengeneza wazazi Hale ambao utatufikisha mahali pazuri.
Aidha pia alimpongeza Mkuu Wa mkoa Wa Arusha Mrisho gambo kwa namna anavyofanya Kazi ya kutekeleza ilani ya chama hicho ,ambapo alisema katika mradi mbalimbali aliyoitembelea ikiwemo ya barabara baipass ,mradi mkubwa Wa maji unaojegwa ndani ya jiji la Arusha ambao utagaeimu kiasi cha shilingi bilioni 520 ,pamoja na mradi Wa Nyuki ambao umebuniwa na Mwenyekiti Wa wazazi mkoa Wa Arusha na unaotekelezwa katika wilaya zote za mkoa Wa Arusha ambapo jumla ya mizinga 700 imwkabidhiwa .
Kwa upande wake Mwenyekiti Wa Ccm mkoa Wa Arusha alisema kuwa baadhi ya wanaccm mkoa Wa Arusha bado wanamakundi lakini akiwa kama Mwenyekiti makundi ayapendi ,na hayataki ,na hata hivyo kuna baadhi ya mambo ambayo hayajakaa sawa ila wameshaanza kuyashulikia .
Aliwaambia wananchi Wa mkoa Wa Arusha wasirilihusu Mbu akaingia katika chama na kuwavuruga na wakimbaini hawatamfumbia macho Bali watamchukulia sheria .
Kwa upande wake Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi mkoa Wa Arusha ambaye ndio ametoa mizinga hii ya Nyuki kwa jumuiya ya wazazi alisema kuwa hii ni moja ya ahadi yake aliyoiadi kipindi akigombea nafasi ya Mwenyekiti Wa wazazi mkoa Wa Arusha
Alisema kuwa mizinga hii itagawiwa katika wilaya zote zilizopo mkoani Hapa na kila wilaya imepatiwa mizinga 100kwa ajili ya wilaya yake,alibainisha kuwa mizinga hii itasaidia kutoa ajira kwa wananchi .
Nae Mkuu Wa mkoa Wa Arusha Mrisho gambo Alisema kuwa ataendelea kushirikiana na chama ili kuahakikisha wananchi wanapata maendeleo ,na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
icha ikionyesha Wa pili kushoto ni Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi Ccm Taifa ambae pia ni mjumbe Wa kamati kuu Edimond mndolwa akimpa mkono Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi mkoa Wa Arusha Herzon mbise wakati wakipandisha moja ya mzinga Wa Nyuki ambao umetokana na mradi Wa jumuiya hiyo ulipo katika Kijiji cha Lorei,kitongoji cha mlimani kata cha Lorei iliopo katika halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru mkoani Arusha ambapo katika mradi huo jumla ya mizinga 100 imetolewa na jumuiya hiyo kwa ajili ya kila wilaya iliopo ndani ya mkoa Wa Arusha (picha na Woinde Shizza ,Arusha).
Meneja Wa Tanroad mkoa Wa Arusha ,muhandisi John kalupale akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti Wa jumuiya ya wazazi Taifa Edimond Mundolwa pamoja na viongozi wengine Wa chama hicho mkoa Wa Arusha wakati alipokuwa akifanya ziara Jana ya kutembelea barabara ya bypass inayotoka kibaoni hadi USA river ,barabara ambayo itapitisha magari makubwa pamoja na mabasi yanayotoka mikoani ikiwemo Namanga ,Singida na Moshi alisema barabara hii itapunguza msongamano Wa magari katikati ya mji (picha na Woinde Shizza, Arusha