Na Silvia Mchuruza,Bukoba
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto Dr.Zainabu Chaula ametembelea chuo cha afya Kagemu kilichopo manispaa ya Bukoba mkoani Kagera na kubaini baadhi ya changamoto zilizopo katika chuo hicho ikiwemo ukosefu wa chakula kwa baadhi ya wanafunzi.
Akizungumza katika chuo hicho Dr. Chaula amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kukabiliana na changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na baadhi ya wanachuo kutokaa na kula chuoni hapo huku akiwataka kuwa wavumilivu wakati suala hilo likishugulikiwa na serikali
Katibu mkuu Chaula amewaeleza wanafunzi hao kwamba kwa chakula cha mchana na usiku kila mmoja wao itabidi kulipia shilingi elfu 1500 .
“Mimi nataka mpate hata chai hapa chuoni ili msome vizuri tutafanya ukarabati wa jiko kwakuwa tayari mna wapishi ili muweze kupata chakula muache kula mtaani ambapo tumekubaliana kila mwanachuo atachanga shilingi 1500 hata hivyo hapa tunatakiwa kufanya utaratibu wa kila mtu amiliki mgomba mmoja ili tusije kupata adha ya chakula”
Baadhi ya wanachuo wameshukuru ujio wa katibu huyo pamoja na jopo lote aliloambatana nalo na kuahidi kwamba watajitaidi katika kutekeleza shughuli mbalimbali za masomo huku wakiahidi kuchangia kiasi hicho cha shilingi elfu 1500.