NA MWANDISHI WETU, TABORA
SHIRIKA la umeme Tanzania TANESCO kupitia idara ya masoko imeanza zoezi la kutoa elimu kwa wananchi wa wilaya na vijiji vya mkoa wa Tabora.
Lengo la utoaji huo wa elimu ni kuwaelimisha wananchi wanaopitiwa na mradi wa REA awamu ya tatu(REAIII) kufahamu taratibu za kuunganishiwa umeme pamoja kuchangamkia fursa za mradi kabla hazijaisha. Miongoni mwa wilaya ambazo tayari zimepitiwa na na sasa ziko kenye zoezi hilo la kupatiwa elimu ni wilaya ya Uyui, Sikonge, na baadae zitafuatiwa na wilaya ya Nzega na Igunga.
Wananchi hao pia walipatiwa elimu kuhusu kifaa cha UMETA yaani umeme tayari anbacho kinafaa kutumiwa na wananchi bila kufanya wiring kwenye nyumba zao hususan zile zinye ukubwa wa wastani w avyumba viwili na sebule.
Wakizungumza wakati wa utoaji elimu kwenye vijiji vya Kagera, Ibiri, Msimba, Msuva, Mtakuja, Songambele na Kasandalala baadhi ya wananchi wamesifu jitihada za serikali za kuwaunganishia umeme kwa gharama ya shilling 27,000/= na tayari badhi yao wameshanufaika na mrafi huo wa umeme.
Aafisa masoko kutoka TANESCO Neema Chalila Mbuja akitoa elimu ya matumizi bora ya umeme na usalama wa umeme Kijiji cha Kagera na Songambele.
Wananchi wa kijiji cha Kagera na Songambele wakifurahia zawadi ya madaftari waliyopewa baada ya kujibu maswali yaliyoulizwa na wataalamu wa TANESCO baada ya kupatiwa elimu hiyo.
Wanakijiji wakifuatilia kwa makini elimu iliyokuwa ikitoelwa kwao kuhusu masuala ya umeme.
Afisa masoko Jenifer mgendi maziku akitoa elimu ya namna ya kutumia kifaa kiitwacho UMETA yaani umeme tayari anbacho kinafaa kutumiwa na wananchi bila kufanya wiring kwenye nyumba zao |