*****************************
Leo katika maadhimisho ya Siku ya Wapendanao (Valentines Day) Tanzania Red Cross Society kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama wamekusanya chupa za damu 343 katika maeneo mbalimbali ambayo zoezi la uchangiaji damu limefanyika.
Mikoa iliyofanya zoezi la uchangiaji damu ni Mkoa wa Mbeya uliokusanya chupa 129, Mkoa wa Dar es Salaam chupa 110, Mkoa wa mara chupa 78, na Mwanza chupa 26.
Mbali na Uchangiaji damu Shughuli mbalimbali za huduma za kibinadamu, upandaji miti, kutembelea wagonjwa na yatima, uhamasishaji na usafi zimeendelea katika sehemu za mikoa ya mwanza, Shinganya Iringa, Geita, Kagera, kigoma, Mtwara Rukwa na kisiwani Unguja.
Akiongoza zoezi hilo Naibu Katibu Mkuu wa Tanzania Red Cross Society Ndg John Busungu amewapongeza wanachama, mavalontia, wananchi na wafanyakazi wa Tanzania Red Cross Society walioshiriki zoezi hili la Uchangiaji damu katika mikoa yote iliyofanya zoezi hili.
Hata hivyo zoezi la Uchangiaji damu litaendelea kesho katika mkoa wa Shinyanga.