Cristiano Ronaldo akiondoka na mpira baada ya kuifungia bao la kusawazisha Juventus kwa penalti dakika ya 90 na ushei katika sare ya 1-1 na wenyeji, AC Milan kwenye mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Italia usiku wa jana Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan. Penalti hiyo ilitokana na Davide Calabria kuunawa mpira wa tik tak wa Ronaldo na refa akatumia VAR kujiridhisha. Milan ilitangulia kwa bao la Ante Rebić dakika ya 61 akimalizia pasi ya Samu Castillejo na sasa timu hizo zitarudiana Machi 4 Uwanja wa Allianz, Torino PICHA ZAIDI SOMA HAPA
RONALDO AINUSURU JUVENTUS KUCHAPWA NA AC MILAN KOMNBE LA ITALIA
By Alex Sonna
February 14, 2020 | 7:52 am

Related Stories
View all
Michezo
1 day ago
CAS YAIREJESHEA SENEGAL UBINGWA WA AFCON 2025
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM Timu ya Taifa ya Senegal imerejeshewa rasmi ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya…
Michezo
2 days ago
MASHINDANO YA KOMBE LA RITTA KABATI YAZINDULIWA KWA KISHINDO WILAYA YA KILOLO
NA DENIS MLOWE IRINGA MASHINDANO ya Kombe la Ritta Kabati 2026 yamezinduliwa rasmi katika Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa, na Mbunge wa Jimbo la…
