Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Dr.Ave Maria Semakafu akifafanua jambo katika mkutano wa tathimini ya mradi wa TESP.
Katibu-Tawala-wa-Mkoa-wa-Arusha-Richard-Kwitega-akifungua-mkutano-wa-wadau-wa-elimu-ya-ualimu.
Picha-ya-Pamoja-ya-Viongozi-na-wadau-wa-elimu-ya-Ualimu-nchini-katika-mkutano-wa-tathmini-ya-mradi-wa-TESP
……………………………………………………………………………………………..
Na Ahmed Mahmoud,Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameipongeza serikali ya Canada kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha elimu ya ualimu nchini kwa kujenga miundombinu ya majengo,TEHAMA na vifaa vya kufundishia pamoja na mafunzo kwa walimu kupitia mradi wa (TESP).
Akisoma risala ya Mkuu wa Mkoa iliyosomwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amepongeza mafanikio ya mradi huo wa elimu unaolenga kukuza ubora wa elimu nchini kwa kuwaandaa walimu bora wataoleta matokeo makubwa kwenye sekta ya elimu nchini.
“Napongeza Uwekezaji wa Tanzania na Canada katika elimu ya ualimu ambayo kuanzia kwenye miundombinu hadi mafunzo kwa ualimu kwani Elimu ni jiko la kupika wataalamu watakaotufikisha kweye ” Alisema Kwitega
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Dr.Ave Maria Semakafu amesema kuwa Mradi huo wamekutana jijini Arusha kufanya tathmini ya utekelezaji wa mradi wa TESP kwasababu huu mradi umejikita katika kuboresha taaluma zaidi,mradi wa kuboresha miundombinu uko katika hatua za mwisho kukamisha.
Pia kuna fedha zinatolewa kwa ajili ya uendeshaji wa vyuo kitaaluma ,kuna fedha zinatolewa kwa ajilli ya wanafunzi.
Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Dkt.Lyabwene Mtahambwa amesema kuwa Mafunzo ya ualimu ni nguzo muhimu katika kuboresha elimu nchini ,tunawaandaa walimu kwa ubora watakaoleta matokeo mazuri .
“Tunawapa mafunzo walimu wawe na upendo kwa wanafunzi na kufanya kazi kwa kujitoa bila kusukumwa ili kufikia mafanikio ya kitaaluma” Alisema Kamishna