Wadau kutoka sekta mbalimbali nchini wametakiwa kujenga tabia ya kufuatilia taarifa za hali ya hewa za mrejeo kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Kujadili jinsi Utabiri wa Mvua za Msimu wa Machi hadi Mei 2020 (MASIKA) utakavyotumika katika Sekta Mbalimbali, uliofanyika tarehe 11 Februari, 2020 katika ukumbi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (The Law School of Tanzania), Dar es Salaam.
“Baada ya mkutano huu, natoa wito kwa wadau kujenga tabia ya kufuatilia mrejeo wa taarifa za hali ya hewa zinazotolewa baada ya utabiri wa awali kutolewa, nasema hivi kwa vile hii ni hali ya hewa, upepo ukibadilika tu na hali ya hewa inabadilika hivyo ni vyema kufuatilia taarifa hizo kwa ukaribu”. Alizungumza Dkt. Nyenzi.
Vile vile, Dkt. Nyenzi alionesha imani yake kwa wadau hao kwamba anatarajia matokeo ya mkutano huo, yatatoa nafasi kwa watanzania kupata utabiri uliokamilika inavyotarajiwa, matumizi yake kiuchumi na kijamii pamoja na athari zinazoweza kutokea na hivyo kuwapa wananchi wasaa wa kujipanga ili kupunguza au kuepusha kabisa madhara.
Awali, wakati akikaribisha wadau hao, Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) aliwashukuru wadau kwa kuitikia mwaliko wa TMA na kuwaeleza kuwa, TMA imejiwekea utaratibu wa kukutana na wadau kipindi cha misimu wa mvua ili utabiri utakaotolewa ukatumike vizuri.
Aidha, kulingana na lengo la mkutano huo, Dkt. Kijazi alielezea kwa kina maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za msimu wa MASIKA, huku akisisitiza utabiri utakaotolewa kutumika kwa faida.
Dkt. Kijazi pia aliwajulisha wadau kuhusiana na mabadiliko ya TMA kisheria na kufafanua jukumu jipya la Mamlaka la kudhibiti shughuli za hali ya hewa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo kutokana na mabadiliko hayo, TMA inaendelea na uboreshaji wa huduma kwa sekta mbali mbali nchini. “Wadau wote wenye vifaa vya
https://www.instagram.com/p/B8cAmdanBmZ/?igshid=10sn1qdyz95ps