NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
WATU 18 wamejeruhiwa kati yao 16 ni wanaume akiwemo mtoto wa miaka tatu ,katika ajali ya basi la abiria kampuni ya SAIBABA kugongana uso kwa uso na lori ,katika barabara kuu ya Morogoro eneo la Kongowe ,Kibaha mkoani Pwani.
Aidha watu watano kati yao hali yao ni mbaya na wanatarajiwa kuhamishiwa hospital ya rufaa ya Taifa ya Mloganzila wakitokea hospital ya Tumbi.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani,Wankyo Nyigesa alisema, mnamo februari 12 majira ya saa moja gari hiyo ya abiria SAIBABA lenye namba za usajili T.779 AVW ikiendeshwa na Richard Wilfred ,ikitokea Sumbawanga kuelekea Dar es salaam ikiwa na abiria ambao idadi yao haijajulikana iligongana uso kwa uso na scania lori yenye namba T.641 DPJ/T.643 DPJ ikitokea Dar es salaam kuelekea Chalinze kubeva kokoto.
Alisema,lori hilo lilikuwa na dereva na utingo wake ambao majina yao bado hayajafahamika na kusababisha majeruhi 18 na katika ajali hiyo hakuna kifo kilichoripotiwa.
“Kati ya majeruhi hao 16 ni wanaume akiwemo mtoto wa miaka mitatu na wanawake ni wawili ,ambapo wote wanapatiwa matibabu hospital ya Tumbi,Kibaha.
Wankyo, alitaja chanzo cha ajali ni dereva wa scania lori kuendesha gari kwa mwendokasi katika eneo lisiloruhusiwa akijaribu kupita magari mengine.
Jeshi la polisi mkoani hapo,linatoa wito kwa madereva kufuata sheria za usalama barabarani na kuzingatia sheria hizo ili kujiepusha na ajali.