Home Biashara Wanafunzi zaidi wanufaika na ufadhili wa masomo kutoka SBL

Wanafunzi zaidi wanufaika na ufadhili wa masomo kutoka SBL

0

Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti (kushoto) na Meneja Mkuu wa Chuo cha Kilimo Kilacha Moshi Vijijini, Jerome Silayo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kusaini mkataba wa ufadhili  wa SBL kwa masomo ya wanafunzi 50 kutoka katika jamii za wakulima kila mwaka kwa kuwalipia ada kwenye vyuo vya kilimo kwa kipindi chote cha masomo yao.  Hafla hiyo imefanyika chuoni hapo leo

Mkuu wa Chuo cha Kilimo Kilacha, Moshi Vijijini, Benito Mwenda, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti na Meneja Mkuu wa Chuo hicho, Jerome Silayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi waliopata ufadhili wa kusomeshwa na SBL.

Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti akiwa na mmoja kati wanafunzi waliopata ufadhili wa kusomeshwa na SBL, Domina Minja 

****************************

Kilacha, FebruarI 12, 2020: Wanafunzi kumi wanaosomea kilimo katika chuo cha Kilacha Agriculture and Livestock Training Center kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro, wamekuwa wa pili kunufaika na ufadhili wa msomo unaotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa wanafunzi wa kilimo hapa nchini.

Chini ya programu yake inayojulikana kama Kilimo-Viwanda, SBL inatoa ufadhili wa masomo kwa wanbafunzi 50 kutoka katika jamii za wakulima kila mwaka kwa kuwalipia ada kwenye vyuo vya kilimo kwa kipindi chote cha masomo yao.

Mwezi uliopita, chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani, kilikuwa ni cha kwanza kunufaika na mpango huo wa ufadhili wa masomo unaolenga kuongeza wataalamu katika sekta ya kilimo hapa nchini.

Akiongea wakati wa zoezi la kutiliana saini lililofanyika chuoni Kilacha, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti alisema programu hiyo inawalenga wanafunzi wanaotoka katika familia za wakulima ambazo hazina uwezo wa kuwalipia ada watoto wao na kuongeza kuwa itasaidia kuongeza wataalamu wa kilimo.

“Tunaamini kuwa programu hii itawasaidia wanafunzi wanaotoka katika familia za wakulima zenye kipato cha chini kupata elimu ya juu huku pia ikichangia kuongeza wataalamu wa kilimo ambao watasaidia kuongeza uzalishaji,” alisema.

Kwa mujibu wa Ocitti, programu hiyo ni sehemu ya mkakati wa SBL wa kuongeza kiasi cha nafaka ambacho kampuni hiyo inanunua kwa ajili ya uzalishaji wa bia ambazo ni pamoja na mahindi, shayiri na mtama. Alisema, mwaka jana SBL ilinunua zaidi ya tani za ujazo 17,000 za nafaka kutoka kwa wakulima wa ndani sawa na asilimia 70 ya mahitaji yake yote ya malighafi kwa mwaka.

“Kampuni ya SBL inalengo la kuongeza kiasi cha malighafi inayonunua kutoka kwa wakulima wa ndani hadi asilimia 85 kufikia mwaka 2020 na ndiyo maana tumeona umuhimu wa kusaidia kusomesha wataalamu wa kilimo ili wakafanye kazi ya kuboresha kilimo chetu. Kwa sasa kampuni inanunua malighafi kutoka kwenye mtandao wenye wakulima 400 hapa nchini,”. alisema

Kwa upande mkuu wa kituo hicho Benito Mwenda aliishukuru SBL kwa ufadhili uliyoutoa na kuzitaka taasisi binafsi kuweza kujitokea na kusaidia sekta ya kilimo ambayo sekta mama.