***************************
Raisi wa Tanzania Red Cross ndugu David Mwakiposa Kihenzile amefika Kilwa mkoani Lindi katika vijiji vya Njinjo na Kipindimbi kuwafariji wahanga wa janga la mafuriko lililo athiri zaidi ya watu 18,000 mwishoni mwa mwezi January mwaka huu.
Itakumbukwa Tanzania Red Cross ilifika mapema sana katika vijiji hivyo na kuanza mara moja kusaidiana na serikali katika kutoa huduma za kibinadamu kwa wahanga ikiwemo utoaji wa mahema na huduma nyingine zakibinadamu.
Akiwa vijijini hapo Njinjo na Kipindimbi Bw Kihenzile ameongoza zoezi la ugawaji wa vifaa mbali mbali kwa wahanga vyenye thamani ya Tsh 120 milioni ikiwemo blanketi 2000, godoro, 2000, kitchen sets 2000, neti, ndoo za maji 200, na vifaa vingine
Aaidha, Rais wa Redcross alitembelea maeneo ya vijiji kushuhudia uharibifu wa makazi na miundombinu uliotokana na mafuriko ya maji katika eneo hilo, ambapo aliambatana na wajumbe mbali mbali wa NEC pamoja na Katibu mkuu Julius Kejo na watendaji wengine wa idara ya maafa ya Tanzania Red Cross.
Mwisho, Rais wa Redcros ameipongeza Idara ya maafa kwa kazi kubwa ya kuongoza voluntia pamoja na wanachama katika kufanya kazi ya kuhudumia wahanga katika kambi hizo za dharura kijijini hapo.