Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Uhamaji (IOM), kanda ya Kusini mwa Afrika Bw. Charles Kwenin akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwaelezea jambo Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Uhamaji (IOM), kanda ya Kusini mwa Afrika Bw. Charles Kwenin akiongea pamoja na Mwakilishi wa IOM hapa nchini Dkt. Qasim Sufi leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa (IOM), Bw. Charles Kwenin, Mwakilishi wa IOM nchini Dkt. Qasim Sufi pamoja na Afisa Uhusiano na Sera wa IOM, Bi. Naomi Shiferaw. Wengine kulia mwa Katibu MKuu ni watumishi wa Wizara, Bw. Hangi Mgaka na Gloria Ngaiza.
…………………………………………………………………………………………………………
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Uhamaji (IOM), kanda ya Kusini mwa Afrika Bw. Charles Kwenin katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yalijadili mambo mbalimbali ikiwemo maandalizi ya Majadiliano kuhusu Uhamaji katika kanda ya Kusini mwa Afrika yanayotarajia kufanyika chini ya uenyekiti wa Tanzania kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Majadiliano hayo yanatarajiwa kufanyika kabla ya mwezi Agosti, mwaka 2020 hapa nchini yakiwa na dhamira ya kujadili usimamizi wa masuala ya uhamiaji ili kuwezesha uundwaji wa sera zenye uwiano miongoni mwa nchi wanachama wa SADC.
Aidha, Balozi Ibuge amewahakikishia wajumbe wa IOM, utayari wa Tanzania kuwa nchi mwenyeji wa Majadiliano hayo.