Mhandisi Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Christopher John akizungumza na walimu Pamoja na wanafunzi wakati Mamlaka hiyo ilipokwenda kutoa elimu ya Mawasiliano katika Shule ya Sekondari Rashid Mfaume Kawawa Wilayani Lindi
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akimkabidhi kitabu cha muongozo wa Mawasiliano Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Rashid Mfaume Kawawa Mohamed Doo wakati Mamlaka hiyo ilipokwenda kutoa Elimu ya Mawasiliano katika Shule hiyo.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wanafunzi na walimu wa Shule ya Sekondari Rashid Mfaume Kawawa Wilayani Liwale wakati wa utoaji wa Elimu ya utumiaji wa Mawasiliano kwa usalama.
Picha ya a pamoja kati ya Watendaji wa TCRA Kanda ya Mashariki na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Anna Magowa.
Picha ya Pamoja kati ya Watendaji wa TCRA Kanda ya Mashariki na wanafunzi wa Shule ya Wasichana Shule ya Sekondari Rashid Mfaume Kawawa Wilayani Liwale mkoani Lindi.
******************************
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Kanda ya Mashariki imetoa elimu ya Mawasiliano katika Shule mbili za Sekondari Wilayani Liwale ili kuwapa elimu ya uelewa Wanafunzi na walimu namna ya kutumia mawasiliano hayo kwa usalama.
Shule za Sekondari zilizipata elimu ya Mawasiliano wilayani Liwale ni Rashid Mfaume Kawawa na Anna Magowa.
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika Shule hizo Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa Wanafunzi wakiwa na elimu ya utumiaji wa mawasiliano ni mabalozi wazuri wa kuelimisha wengine pamoja na wao wakifikia umri wa kumiliki simu na bidhaa zingine za Mawasiliano watakuwa wanatumia kwa usalama.
“Ninaamini Wanafunzi wetu wakipata elimu ni hakika wataweza kuelimisha wengine utumiaji wa mawasiliano kwa usalama pamoja na wao kuwa kizazi bora wakati wakiwa wametimiza umri wa kumiliki simu kuzingatia matumizi salama ya utumiaji wa simu hizo na huduma mbalimbali za mitandao”amesema Mhandisi Odiero.
Mhandisi Odiero amesema kuwa TCRA ndio wadhibiti wa mawasiliano hivyo wanawajibu wa kuwalinda watumiaji katika matumizi salama ya Mawasiliano.
Aidha amesema kuwa utoaji wa elimu hiyo ni endelevu kutokana na teknolojia ya Mawasiliano kubadilika kila wakati hivyo TCRA lazima iendane na mabadiliko hayo.
Nae Mkuu wa Shule wa Rashid Mfaume Kawawa Mohamed Doo amesema kuwa kwa elimu waliopata wataitumia kuelimisha wengine pamoja na wanafunzi kuwa mabalozi katika jamii wanayoishi.
Amesema kuwa TCRA imethubutu katika utoaji wa Elimu ya Mawasiliano katika makundi mbalimbali nia ni kuwa na matumizi salama ya Mawasiliano.
Kwa upande wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Anna Magowa amesema TCRA wamefika wakati mwafaka kutokana wa kuelimisha namna ya kutumia Mawasiliano salama ya simu na mitandao mbalimbali.