Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na Watalii wa ndani katika Tamasha lililofanyika katika kisiwa cha Sinda katika wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa lengo kuamsha ari ya wananchi kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) pamoja na Mdau wa Utalii, Michael Mbano ( katikati) wakisafiri kwenye boti kuelekea katika kisiwa cha Sinda ambako Tamasha la Utalii lililowakutanisha Manaibu Waziri wa tatu akiwepo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Mhe. Abdallah Ullega kwa lengo la kuhamasisha utalii wa ndani lililofanyika katika kisiwa hicho kilichopo katika wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda, Dkt.Damas Ndumbaro akimkabidhi cheti cha shukrani kwa kudhamini Tamasha la Utalii wa ndani Mwakilishi wa Kampuni ya Pepsi katika Tamasha hilo lililofanyika katika Kisiwa cha Sinda na kuhudhuriwa na zaidi ya Watalii wa ndani wapatao 100 pamoja na Manaibu Waziri watatu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu( wa pili kulia) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Abdallah Ulega ( wa tatu) pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa nne) wakisaini vitabu vya wageni kabla ya kuanzia kuzungumza na Watalii wa ndani katika Tamasha lililofanyika katika Kisiwa cha Sinda
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega wakizungumza na Meneja wa Kisiwa cha Sinda, Bw.John Komakoma Wakati walipokuwa wakiwasili katika kisiwa hicho jijini Dar es Salaam.
Manaibu Waziri watatu wakiwa na baadhi ya Watalii wa ndani walioshirikia Tamasha la Utalii wa ndani lilioandaliwa na Kampuni ya Watalii ya Siga Tours and Travel Agency katika Kisiwa cha Sinda kilichopo katika wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda Dkt.Dramas Ndumbaro akimkabidhi cheti cha pongezi, Emma Sizzy ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Siga Tours and Travel Agency mara baada ya Manaibu Waziri kuzungumza na na Watalii wa ndani zaidi 100 waliokuwepo katika Kisiwa cha Sinda.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda Dkt.Dramas Ndumbaro akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakiwa pamoja na baadhiya watumishi wa kisiwa hicho.
Muaandaji wa Tamasha la Utalii wa ndani na miliki wa Kampuni ya Utalii ua Siga Tours and Travel Agency akizungumza mbele ta Manaibu Waziri watatu huku akiwaomba kumpa Ushirikiano ili kuweza kuhamasisha Utalii wa ndani
…………………………………………………………………………………….
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema juhudi zinazofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wadau wa utalii nchini ni moja ya hatua muhimu ya kuihamasisha jamii kuona thamani ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini badala ya kutegemea Watalii kutoka nje.
Aidha, Mhe.Kanyasu amesema juhudi hizo zinaenda sambamba na kuhamasisha jamii kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kiuchumi katika maeneo ambako shughuli za kitalii zinafanyika badala ya kudhani kuwa Watalii wanaokuja kwa ajili ya kutembelea vivutio vya Utalii wanakuja kwa ajili ya kuhodhi njia za kiuchumi
Akizungumza leo na Watalii wa ndani wapatao 100 katika kisiwa cha Sinda kilichopo katika wilaya ya Kigamboni Jijin Dare s Salaam, Mhe.Kanyasu amesema kuimarika kwautalii wa ndani kutaifanya jamii kuwaona Watalii wa kutoka nje ya nchi ni fursa kutokana na mzunguko wa pesa kutoka kwa Watalii kwenda kwa jamii.
Katika Tamasha hilo la kuhamasisha Utalii wa ndani wa ndani lililowakutanisha Manaibu Waziri watatu akiwemo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu, Naibu Waziri wa Mambao ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda, Dkt. Damas Ndumbaro pamoja na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega
Mhe. Kanyasu amesisitiza ” Tunataka jamii ikiona Mtalii ameibiwa au ameporwa jamii isikitike na kuona fursa za kiuchumi zinatoweka kupitia mtalii aliyetendewa vibaya”
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda, Dkt.Dramas Ndumbaro amesema sekta ya Utalii ni sekta mtambuka na Watalii wanapotembelea vivutio vya Utalii jamii nzima inafaidika
Kutokana na hilo, Naibu Waziri Ndumbaro ameitaka jamii kuacha kuposti vitu visivyofaa kwenye mitandao ya kijamii vya kuichafua nchi badala yake jamii itangaze vivutio vya Utalii vilivyopo nchini.
” Tangazeni vivutio vya Utalii ili watu wa nje waweze kufahamu vivutio vyetu vilivyopo nchi ni” alisisitiza Dkt.Ndumbaro.
Naye, Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo, Mhe.Abdallah Ulega amesema Utalii wa fukwe ni utajiri wa Watanzani wote hivyo jamii ijitokeze kutembelea fukwe hizo.
Amesema ni muhimu jamii kuona ufahari wa kutembelea visiwa vilivyotunzwa kwa ajili ya kupumzika na kujiburudisha baada ya kukamilisha majukumu mazito ya kila siku.
Naye, Mmiliki wa Siga tours and Travel Agency ambaye ni Muaandaji wa Tamasha hilo la Utalii wa ndani, Emma Sizzya ametoa wito kwa Wadhamini wenye ni ya kudhamini matamasha ya Utalii wa ndani wajitokeze kusaidia hili kuhamasisha Utalii wa ndani.
” Sisi hatuhitaji fedha tunachohitaji ni utayari wako kusaidia ili kuamsha ari ili jamii iweze kuhamasika na Utalii wa ndani, alisisitiza Muaandaji wa Tamasha hilo, Emma Sizzy
” Sisi hatuhitaji pesa tunachohitaji kutoka kwa Wadhamini ni msaada wa kile anachozalisha kitakachosaidia kufanikisha tamasha la Utalii kuweza kufanyika