Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe,akizungumza na wadau wa zao la zabibu kwenye kikao cha kujadili changamoto mbalimbali zinazolikumba zao hilo hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe.Mwanahamisi Munkunda akizungumza kwenye kikao cha wadau wa zao la zabibu chenye lengo la ujadili changamoto mbalimbali zinazolikumba zao hilo kilichofanyika ijini Dodoma.
Sehemu ya wadau wa zao la Zabibu wakifatilia majadilianao na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe, kwenye kikao cha kujadili changamoto mbalimbali zinazolikumba zao hilo hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma.
MKurugenzi wa Doniya Estate ambaye msindikaji wa zao la zabibu Catherine Mwambie,akitoa maoni yake kwa Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe,alipokutana na wadau wa zao la zabibu kwenye kikao cha kujadili changamoto mbalimbali zinazolikumba zao hilo hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma.
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
……………………………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe,ameunda timu ya watu 12, huku ikiwapa siku 10 kuhakikisha wanafanya utafiti wa zao la Zabibu kama linaleta hasara au faida kwa mkulima na kwa serikali.
Aidha timu hiyo pia imeagizwa kujua magonjwa yanayoathiri zao hilo na kujua mkulima akipanda heka moja inamgharimu kiasi gani. Hii itasaidia kupata takwimu sahihi ya gharama anazopata mkulima kwenye uzalishaji kwani kilimo cha zabibu kina gharama kubwa.
Mhe.Bashe ameyasema leo jijini Dodoma alipokutana na kuongea kwenye Mkutano wake na wadau wa zao la zabibu walipokuwa wakijadili changamoto mbalimbali zinazoikabili zao hilo.
“Zao la zabibu hapa Dodoma linakua kwa kudra za Mwenyezi Mungu, ndio maana nimeamua kuunda, ‘technical team’ ili iweze kuleta ripoti tutakayoifanyia kazi”.amesema Bashe
Bashe amesema kuwa zao la zabibu ndio uti wa mgongo wa Jiji la Dodoma hivyo Kuna Kila sababu ya kuweka mpango mkakati kwa ajili ya kuinua zao Hilo. Bashe ameunda kamati ya watu 12 itakayoongozwa na Mkurugenzi msaidizi kutoka ofisi ya Sera na Mipango kwa upande wa Sera akiwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambapo wote watafanya utafiti kwa muda wa wiki moja na kuwasilisja ripoti.
“Ripoti itakayoletwa na kamati hii,itatusaidia kujua wakulima wa zabibu wako wangapi? Changamoto za Wakulima,wazalishaji na wasindikaji, hivyo itatusaidia katika mikakati yetu”‘amesisitiza Bashe.
Aidha Bashe amesema kuwa, mkakati mwingine wa Serikali ni kufufua mabwawa yote yaliyotengenezwa kwa ajili ya umwagiliaji wa zabibu katika Wilaya tatu zinazolima zao hilo ambazo ni Bahi,Chamwino na Dodoma.
Bashe amewataka wadau wa Kilimo Cha zabibu kuunda Vyama vya Ushirika ili viweze kusaidiwa kwa karibu na Taasisi za Fedha.
Naye MKurugenzi wa Doniya Estate ambaye ni msindikaji wa zao la zabibu Catherine Mwambie amesema kuwa suala la Kodi limekuwa kikwazo kikubwa kwa wazalishaji wa mvinyo.
“Yaani kwa siku moja zinakuja Taasisi zaidi ya Tano Kila moja inakuja kuchukua Kodi, sasa tunajikuta hata faida hatupati, maana hela yote inaishia kwenye hizo Kodi” amesema Mwambie.
Aidha Mwambe amesema kuwa, gharama za uzalishaji ziko juu, na Soko la zabibu hapa nchini bado,hivyo waniomba Serikali kuingilia Kati,kuweka mazingira rafiki ya biashara ya zabibu.