Home Mchanganyiko RAIS MAGUFULI KUZINDUA RASMI WILAYA YA KIGAMBONI KESHO

RAIS MAGUFULI KUZINDUA RASMI WILAYA YA KIGAMBONI KESHO

0
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho February 11 kuanzia Saa Mbili Asubuhi anatarajiwa Kuzindua Rasmi Wilaya Mpya ya Kigamboni ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa Wingi katika Uzinduzi huo wa Kihistoria.
RC Makonda amesema hafla ya Uzinduzi huo inatarajiwa kuanza Saa Moja Asubuhi kwenye Viwanja vya Mkuu wa Wilaya ambapo Rais Magufuli atazindua Jengo la Utawala la Mkuu wa Wilaya, Jengo la Halmashauri na Majengo ya Hospital ya Wilaya ya Kigamboni.
Uzinduzi huo unakuja wakati muafaka ambao Tayari Serikali imefanya juhudi kubwa za Maendeleo katika Wilaya hiyo kupitia Miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Barabara za Lami, Ujenzi wa Hospital, Vituo vya Afya, Zahanati, Huduma za maji, Elimu pamoja na huduma zote muhimu.