Vijana wa vyuo vikuu wakimsikiliza Katibu wa itikadi na uenezi Taifa , Humphrey Polepole leo jijini Arusha.(picha na Happy Lazaro).Polepole akiongea kwenye mkutano huo.
************************
Happy Lazaro,Arusha.
Katibu Mwenezi Taifa ambaye ni mlezi wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Ndg Hamphrey Pole pole amewataka vijana wa vyuo vikuu Mkoani Arusha ambao wanagombea nafasi mbalimbali za uongozi, kufuata maadili ya uongozi ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano
Ameyasema hayo Leo katika hotel ya Naura spring, katika Darasa la itikani kwa Wanafunzi wa vyuo na Vyuo vikuu iliyofanyika Jijini Arusha kwa lengo la kuwapa uelewa wa chama cha Mapinduzi na taratibu zake kwa ujumla.
Aidha aliwasisitizia kuwa Chama cha Mapinduzi kina lenga kuwataka vijana kuwa na maadili na kutumia mitandao ya kijamii katika kujenga Chama na sio kutumia kughushi habari za uongo.
Hata hivyo amewataka vijana hao kuendelea kusoma ili kujiongezea maarifa ili kupata ufahamu wa taarifa mbalimbali zinazohusu chama na serikali.
Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Jerry Muro amesema kuwa vijana hao wakawe chachu ya ushindi kwa ccm katika Mkoa wa Arusha ili kumuenzi Rais Dr John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri alivyofanya katika awamu yake ya kwanza ya Uongozi ikiwemo, sekta afya, Elimu, miundombinu pamoja na sekta ya Anga.