Home Mchanganyiko CHALINZE YAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA SH BIL.40.8 KWA MWAKA 2020/2021

CHALINZE YAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA SH BIL.40.8 KWA MWAKA 2020/2021

0

NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze limepitisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa  fedha 2020/2021 ya zaidi ya sh.bil 40.8.
Mapendekezo hayo ni sawa na ongezeko la sh. bil 4.655.3  ukilinganisha na bil 36,231,664,877 iliyoidhinishwa kutumika katika mwaka wa fedha 2019/2020 ambayo ni ongezeko la asilimia 12 ya bajeti iliyopendekezwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Amina Kiwanuka, alieleza hayo katika kikao cha baraza la madiwani kupitisha mapendekezo hayo ya bajeti  kilichoketi Mjini Lugoba.
Alisema, ongezeko hilo limetokana na marekebisho yaliyofanyika katika vyanzo vya mapato  vya ndani,  na Ruzuku ya mishahara ambayo Halmashauri imeongeza naksi ya mapato ya ndani kutoka bil 6.167.9 hadi kufikia bil 8. 156.450 kiasi ambacho ni ongezeko la bil 1,988,550,870.
Kiwanuka ameeleza, ugawaji wa mapato ya sh.bil 40.886.9 katika matimizi ya mwaka  2020/2021 vimezingatia vipaumbele katika Sekta ya elimu, kuboresha miundombinu ya shule za Msingi na Sekondari na katika Afya kuongeza miundombinu.
Alisema, kwa upande wa matumizi ya mapato ya ndani, Halmshauri hiyo inatarajia kutumia kiasi cha sh.bil 8,156,450,870 ambapo kiasi cha shilingi Bilion 4,893,870,522 sawa na asilimia 60 ya fedha zisizo na masharti kitatumika kwa miradi.
Aidha alibainisha, sh.bilioni 3,262,580,348 sawa na asilimia 40 ya fedha zisizo na masharti zitaelekezwa katika matumizi ya kawaida  na kwamba bil 2.666.762zitapelekwa katika miradi ya maendeleo yenye masharti.