Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mtela Livingstone Lusinde wakisalimiana na wananchi mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kuzindua Mradi wa Maji Safi katika kijiji cha Makang’wa uliogharamiwa na Wizara ya Maji na kutekelezwa na DUWASA katika Jimbo la Mtera mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi David Pallangyo,akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi katika kijiji cha Makang’wa uliogharamiwa na Wizara ya Maji na kutekelezwa na DUWASA katika Jimbo la Mtera mkoani Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Mtela Livingstone Lusinde,akizungumza na wananchi kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi katika kijiji cha Makang’wa uliogharamiwa na Wizara ya Maji na kutekelezwa na DUWASA katika Jimbo la Mtera mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso,akizungumza na wananchi wa Makang’wa kabla ya kuzindua wa Mradi wa Maji Safi katika kijiji cha Makang’wa uliogharamiwa na Wizara ya Maji na kutekelezwa na DUWASA katika Jimbo la Mtera mkoani Dodoma.
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Makang’wa wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Maji Mhe.Aweso Juma alipokuwa akiwahutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi katika kijiji cha Makang’wa uliogharamiwa na Wizara ya Maji na kutekelezwa na DUWASA katika Jimbo la Mtera mkoani Dodoma.
Vikundi mbalimbali vya Kwaya vikitoa burudani kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi katika kijiji cha Makang’wa uliogharamiwa na Wizara ya Maji na kutekelezwa na DUWASA katika Jimbo la Mtera mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso,akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi na Meneja wa Ufundi Duwasa Mhandisi Kashilimu Mayunga,akimuonyesha ramani ya Mradi wa Maji Safi katika kijiji cha Makang’wa uliogharamiwa na Wizara ya Maji na Kutekelezwa na DUWASA kwenye Jimbo la Mtera mkoani Dodoma
Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso,akizundua Mradi wa Maji Safi katika kijiji cha Makang’wa uliogharamiwa na Wizara ya Maji na kutekelezwa na DUWASA katika Jimbo la Mtera mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso akiwa na Mama wakiwa wamebeba ndoo ya maji mara baada ya kuzindua wa Mradi wa Maji Safi katika kijiji cha Makang’wa uliogharamiwa na Wizara ya Maji na kutekelezwa na DUWASA katika Jimbo la Mtera mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mtela Livingstone Lusinde wakiwa wamebeba Ndoo ya Maji kuashiria kuwa uzindua wa Mradi wa Maji Safi katika kijiji cha Makang’wa uliogharamiwa na Wizara ya Maji na kutekelezwa na DUWASA katika Jimbo la Mtera mkoani Dodoma umekamilika na wananchi wameshaanza kupata maji.
Wananchi wakicheza kwa kufurahia mara baada ya kupata maji Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso ambaye amezindua Mradi wa Maji Safi katika kijiji cha Makang’wa uliogharamiwa na Wizara ya Maji na kutekelezwa na DUWASA katika Jimbo la Mtera mkoani Dodoma.
PICHA PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
……………………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Mtera
Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso,amewataka wananchi wa Kata ya Makang’wa kuutunza mradi wa maji wenye thamani ya sh milioni 350 ambao unatoa lita 379,200 kwa siku zenye uwezo wa kuhudumia wakazi 7555 wa kata hiyo.
Na pia amekabidhia sh milioni 100 kwa ajili ya kuongeza visima vingine viwili katika Kata hiyo ambavyo wataalamu wa Maji watafanya utafiti kujua wapi vichimbwe.
Wito huo ameutoa jana wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa maji safi katika kijiji cha Makang’wa uliogharamiwa na Wizara hiyo na kutekelezwa na Duwasa,amesena kuwa kupitia Force Account inafanikisha kujenga miradi ya maji vijijini na mijini na kuokoa kero za maji kwa wananchi.
Mhe.Aweso ametoa pongezi kwa Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira Duwasa kutokana na kutekeleza mradi huu kwa muda mfupi kwa gharama nafuu toafuti kama tungemkabidhi mkandarasi.
”Natoa pongezi zangu kwako Mhandisi Pallangyo kwa sababu wewe na wataalamu wako mmefanya kazi kubwa mno kwa kuwapatia maji wakazi wa eneo hilo, “amesema Aweso.
Aidha Mhe.Aweso ameiagiza kamati ya maji ya kata hiyo kuhakikisha inatoa ripoti ya mapato na matumizi ya fedha ambazo watauza maji kupitia mradi huo.
“Sitaki kusikia marumbano ya mradi huu taarifa za mapato na matumizi ya mradi lazima zisomwe kwa wananchi ili waweze kujua, “amesisitiza Aweso
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi David Pallangyo amesema kabla ya kutekelezwa kwa mradi huu hali ya maji katika Kata hiyo haikuwa ya kuridhisha.
Mhandisi amesema kuwa maji ya bomba yalikuwa yanapatikana katika kitongoji kimoja cha Sasi kati ya vitongoji 11 vya Makang’wa ambayo yalikuwa hayatoshelezi kabisa kwa wakazi wa eneo hilo na yaliwekwa na mtu binafsi.
“Wananchi wa karibu na eneo hilo walikuwa wanafuata maji kwenye kitongoji hicho kwa sh 200 kwa ndoo ya lita 20,lakini hivi sasa maji ya DUWASA ndoo mbili watalipia sh 50,”amesema Mhandisi Pallangyo.
Hivyo DUWASA imefanikiwa kumtua ndoo Mama kichwani kama kampeni yetu inavyosema.
Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Mtela Livingstone Lusinde amemshukuru Naibu Waziri kwa kuwapatia maji wakazi wa eneo hilo na kuondoa kero ya maji toka miaka 50 iliopita.
”Mimi kama Mbunge nitashirikiana na wananchi kuhakikisha tunautunza mradi huo ili uendelee kutoa maji kila siku”amesema Mhe Lusinde