………………………………………………………………………………………………
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
TUME ya Taifa ya Uchaguzi ,tayari imekamilisha maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ,katika kundi la mkoa wa Dar es salaam na Pwani .
Aidha, kwasasa Tume hiyo inaendelea na zoezi la kuhamasisha wadau kwa kutoa semina katika ngazi za mkoa,Jimbo na kata.
Akifungua mkutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wadau wa uchaguzi, Makamu Mwenyekiti wa Tume ,Jaji Mbarouk Mbarouk, huko Kibaha Mkoani Pwani ,alifafanua ,zoezi la majaribio lilifanyika katika mikoa ya Pwani na Morogoro kama sehemu ya maandalizi ya uboreshaji daftari .
“Katika mkoa wa Pwani uandikishaji huo ulifanyika katika kata ya Kibuta wilayani Kisarawe na Morogoro ulifanyika kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro.”:
Hata hivyo,uboreshaji unaendelea katika halmashauri saba za mkoa wa Morogoro.
“:Lengo la uandikishaji wa majaribio ulifanyika kwa siku saba kuanzia machi 29 mwaka jana hadi april 4 ,lilikuwa ni kupima uwezo wa mfumo wa uandikishaji na utendaji kazi wa vipuri vipya vilivyofungwa kwenye mashine za kielektroniki za BVR.:”alibainisha Mbarouk.
Mbarouk aliwashukuru wananchi wa Kibuta ,na kuwaomba wajitokeze tena kwa wingi katika kipindi hiki cha zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura.
Pamoja na hayo ,alisema kwamba uboreshaji umeshakamilika pia mikoa 23 ya Tanzania Bara,halmashauri mbili za mkoa wa Morogoro na mikoa yote mitano ya Tanzania Zanzibar.
Alieleza Mbarouk ,Tume ya Taifa imepewa jukumu la kikatiba la kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa Rais na wabunge na madiwani ikiwa ni kwa mujibu wa ibara ya 74(6) (a) na (d) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.
Pia alisema ,Tume inatambua umuhimu wa kuwashirikisha wadau katika michakato ya uchaguzi kwa lengo la kuwa karibu nao,kujenga imani kwa jamii na kuweka uwazi katika utekelezaji wa majukumu yake.
Mada kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ,iliyoandaliwa na mkurugenzi wa uchaguzi ,dkt Wilson Mahera ilielezea ,zoezi la uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura nchi nzima lilifanyika 2018,Lengo lilikuwa kuona kama vituo hivyo bado vipo na kama bado vina sifa na hadhi kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.
“Kutokana na uhakiki huo vituo vya kuandikisha wapiga kura kwa nchi nzima viliongezeka kutoka 36,549 hadi 37,407 lakini kwa mkoa wa Pwani vituo hivyo 1,734 vya kuandikishia wapiga kura vilivyokuwepo mwaka 2015 na havijaongezeka kwa mwaka huu”alisema
Katika hatua nyingine, Mahera alieleza ,uboreshaji huu unahusisha waliofikisha miaka 18 mwaka huu, waliohama kuhamia maeneo mengine na waliopoteza kadi na kupoteza sifa.
Kwa upande wake ,ofisa uhamiaji ,kamishna msaidizi Wilfred Minja akieleza elimu ya uraia ,alisema masharti ya mpiga kura lazima awe raia wa Tanzania ,ambae amezaliwa na wazazi aidha mmoja awe Mtanzania au kazaliwa Zanzibar.
Alisema, ambae amezaliwa na wazazi ambao sio raia wa Tanzania awezi kuwa raia mfano ,wakimbizi hata kama watoto wao wamesoma Tanzania lakini watakuwa hawana sifa ya kuwa raia wa Tanzania .
Zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura ,linatarajia kuanza februari 14- na kukamilika februari 20 mwaka huu.