Na Jozaka Bukuku
TAASISI
ya Tanzania Growth Trust (TGT) imeandaa maonesho ya wajasiriamali ambayo
yanatarajia kufanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam
kuanzia Februali 24 hadi 28 mwaka huu.

TGT
katika kilele cha programu zake imekuwa na utaratibu wa kila mwaka kuandaa
maonesho ya wajasiriamali ambao wamepitia kwenye mikono yao wakati wa mafunzo
na malezi huku pia wakishirikisha wajasiriamali wengine nao kushiriki.

Lengo
la kufanyika kwa maonesho haya ni kupanua masoko ya wajasiriamali hapa nchini
na kuwanjengea uzoefu waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora na zinazokidhi
viwango vya Kimataifa.

Ili
kuhakikisha malengo haya yanatimia TGT hufanya ukaguzi wa kina kutazama bidhaa
ambazo zimezalishwa na wajasiriamali waliopitia mafunzo yao wakati wa maonesho.

kupitia Programu ya MKUBWA imekuwa ikitoa mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi
wa biashara kwa wanawake ambapo wamekuwa wakipatiwa fursa ya kujifunza
kuzalisha bidhaa,kutafuta masoko,usimamizi wa fedha na urasimishaji wa biashara
zao.

Miongoni
mwa fani zinazowekewa mkazo na TGT wakati wa mafunzo ni pamoja na ushonaji na
ubunifu wa mavazi,ufugaji wa kuku, uzalishaji wa batiki, sanaa za mikono na
usindikaji wa vyakula.

Kazi
hii imekuwa ikifanyika kwa kushirikiana na Taasisi za Umma ambazo
zinashughulika na masuala ya urasimishaji wa biashara zikiwemo BRELLA, SIDO,
TMDA, TRA na nyinginezo.

Akizungumza
kuhusiana na maonesho ya MKUBWA, Afisa Mtendaji Mkuu wa TGT, Bi Anna Dominick
amesema kuwa kwa muda mrefu sasa maonesho haya yamekuwa kimbilio la
wajasiriamali wengi hapa nchini wanaotafuta masoko ya bidhaa na huduma
wanazotoa.

“Maonesho ya siku ya MKUBWA yamekuwa na
matokeo chanya kila mwaka kwani wapo baadhi ya wajasiriamali ambao kupitia
uzoefu walioupata TGT wamekuwa wakipeleka bidhaa zao kwenye maonesho ya
Kimataifa nje ya nchi”alisema Bi Dominick.

“Tulilazimika
kuwajengea mazingira ya kujiamini ndani ya nchi kupitia MKUBWA lakini hivi sasa
wamepiga hatua na wapo ambao bidhaa zao zimeanza kushika kasi kwenye masoko ya
Kimatafa.Hiki ni moja kati ya vitu ambavyo tunajivunia”alisema Afisa Mtendaji
huyo.

Bi Anna alimaliza kwa kuwaalika Watanzania
kujitokeza kwa wingi kila mwaka yanapotangazwa maonesho hayo ili kuwaunga mkono
wajasiriamali ambao wanazalisha bidhaa zao kutokana na malighafi za ndani
Afisa Mtendaji mkuu wa
TGT, Bibi Anna Dominick akiwa kwenye moja ya mikutano ya Taasisi hiyo.
Wanufaika wa mafunzo ya
ujasiriamali chini ya program ya TGT MKUBWA wakiwa kwenye maonesho.