Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Ditopile (kulia) akikabidhi Kompyuta kwa viongozi wa UVCCM Mkoa wa Tanga lengo likiwa kusaidia ufanisi wa kazi zao.
Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Ditopile (kulia) akimkabidhi kiasi cha fedha Mkuu wa Gereza la Korogwe, Daud alipofika kuwatembelea wafungwa wa Gereza hilo.
Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Ditopile akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa UVCCM Mkoa na wengine kutoka Wilaya mbalimbali za Mkoa huo.
……………………………………………………………………………………………………………..
Katika kusherehekea miaka 43 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM, Mbunge wa Viti Maalumu Vijana, Mariam Ditopile amekabidhi Kompyuta 10 zenye thamani ya Sh Milioni Tano kwa viongozi wa UVCCM Wilaya zote za Mkoa wa Tanga.
Pia ameahidi mifuko 20 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Korogwe ambapo kuna changamoto ya uzio jambo ambalo linasababisha wakina Mama wanaojifungua kukosa faragha kwani kituo hiko kipo karibu na barabara kubwa.
Mhe Ditopile akiambatana na vijana wa UVCCM Ditopilewametembelea pia Gereza la Korogwe ambapo waliwagawia vifaa vya Usafi pamoja na kuwafariji.
Akizungumzia mafanikio ya Serikali, Ditopile amesema ndani ya kipindi cha miaka nne ya uongozibwa Rais Magufuli Nchi imepiga hatua kubwa katika maeneo yote muhimu ambayo yanagusa maisha ya wananchi.
Amesema chini ya uongozi wa Rais Magufuli tatizo la watoto wa maskini kukosa elimu kwa sababu ya ukosefu wa karo ya shule limekwisha kabisa kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha nne kwani takribani Bilioni 21 zimekua zikilipwa na serikali kila mwezi kwa ajili ya Elimu bila malipo.
” Vijana ndio tunapaswa tusimame tuzungumzie mafanikio ya Mhe Rais Na serikali yake katika kuwatumikia watanzania hasa wanyonge, kila sekta imeguswa leo watoto wetu wanasoma bure hadi kidato cha Nne kwa ada inayolipwa na Rais kiasi cha Bilioni 21 kila mwezi.
Nchi nyingi zimekuja kujifunza kuhusu elimu bure kwetu, zipo Nchi zimekuja pia kujifunza kuhusu mradi wa umeme vijijini REA. Tanzania inapiga hatua kwenye kila nyanja, kwenye madini leo tunagawana na wawekezaji 50/50. Yote haya yamefanikiwa kwa sababu ya usimamizi thabiti wa mzalendo Dk John Magufuli, ” Mhe Ditopile.
Mbunge Ditopile amewataka watanzania kumuunga mkono Rais Magufuli kutokana na utendaji kazi wake ambao umeacha alama kubwa sana ndani ya kipindi kifupi.