WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kusimamishwa kazi kwa mtumishi wa Halmashauri ya Kilosa mkoani Morogoro Daniel Elimringi, kutokana na kuchana kitabu cha Dini.
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
………………………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ameagiza kusimamishwa kazi kwa mtumishi wa Halmashauri ya Kilosa mkoani Morogoro Daniel Maleki, kutokana na kuchana kitabu cha Dini.
Aidha ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike ili mamlaka za kinidhamu zichukua hatua dhidi ya kitendo hicho kilichofanywa na mtumishi huyo
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo mara baada ya kusambaa kwa picha katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikimuonyesha mtumishi huyo katika Halmsahauri ya Kilosa kitengo cha biashara idara ya fedha akichana na kutupa kitabu cha dini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Mhe.Jafo amesema kuwa amechukua hatua hiyo kwa sababu Elimringi ni mtumishi ambaye yupo chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI.
“Kitendo hicho cha kuchana kitabu cha dini, hakileti afya njema kwa taifa letu ambalo wananchi wake wamekuwa wakiheshimiana kiimani.
Hata hivyo Jafo amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Morogoro, pamoja na mkuu wa Wilaya ya Kilosa, kusimamia suala hilo na kuendelea kulinda amani na utulivu uliopo nchini.