*********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Yanga leo imefanikiwa kuondoka na pointi zote tatu baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya lipuli Fc mabao 2:1 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Yanga ilifanikiwa kupata bao la kuongoza kipindi cha kwanza kupitia kwa kiungo mshambuliaji wao Balama Mapinduzi akipokea krosi kutoka kwa Juma Abdul na kupiga kichwa na kufanikiwa kuitanguliza timu yake kuongoza mnamo dakika ya 14.
Hata huivyo Yanga ilionekana kuzidi kulisakama lango la timu pinzani hivyo iliwachukua dakika 32 kupata bao lingine lililowekwa kimyani na Bernard Morrison na hadi mapumziko yanga ilikuwa ipo mbele kwa mabao 2:0.
Kipindi cha Pili nao Lipuli walianza kulisakama lango la Yanga na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi mnamo dakika 58 kupitia kwa mchezaji wao David Mwasa.