Baadhi ya wadau wa Bonde la mto Katuma katika jukwaa la tatu la kidakio cha mto Katuma kilichofanyika katika manispaa ya Mpanda
…………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu, Katavi
Wadau mbalimbali kutoka katika asasi za kijamii wameishauri Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Rukwa kuweka mipaka inayoonekana katika vyanzo vya maji ili kurahisisha uelewa wa mipaka hiyo kwa wananchi na hivyo kuepusha migogoro isiyo ya lazima
Wametoa ushauri huo katika jukwaa la tatu la wadau wanaotumia maji katika kidakio cha mto Katuma unaotiririsha maji katika Ziwa Rukwa; kilicholenga kuendeleza utunzaji wa rasilimali za maji
“Kama tutafyeka kama TANAPA wanavyofanya ni rahisi kwa mtu kuona mbona hapa pamefyekwa na kule kumehidhawa, kwahiyo atajua kumbe kule ni hifadhi tungefanya hivyo hata kwa bonde la mto Mpanda” alisema mama Fulgensia Kapama kutoka asasi ya wanawake ya KAWODEO
Aidha wadau hao wamependekeza kuwepo na sheria za ndogo kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji
Akitolea mfano wa hifadhi ya jamii ya Mpimbwe mkurugenzi wa taasisi ya UDESSO bwana Eden Waimba ameiomba serikali na wadau mbalimbali kuongeza nguvu katika kuilinda hifadhi hiyo
“Kule kuna wanyama pori kwahiyo ni chanzo cha mapato pia kwa taifa; ila sasa imeanza kuingilia na shughuli mbalimbali za kibinadamu” alisema
Bwana Thadeus Ndeseiyo ni Mjumbe wa Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Rukwa; amesema kuna umuhimu mkubwa wa kutunza vyanzo vya maji kwa manufaa ya viumbe hai